Friday, April 1, 2016

WAZIRI LUKUVI AZITAKA HALMASHAURI KUWASILISHA ORODHA YA MASHAMBA PORI AMBAYO HAYAJAENDELEZWA.




Waziri  ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mh Wiliam Lukuvi amezitaka halmashauri kutimiza majukumu yake kwa kuwasilisha kwake orodha ya mashamba pori ambayo hayajaendelezwa ili hatua za  kufuta vibali vya umiliki wake zifanyike na siyo kubaki kulalamika kuwa kuna mashamaba makubwa ambayo hajaendelezwa na hivyo kuwanyia haki wakulima na wafugaji kufanya shughuli zao.

Mh.Lukuvi ameyasema hayo alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi  Maliasili na Utalii alipokutana na  uongozi wa mradi wa urasilimishaji ardhi Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhandisi Atashasta Nditiye amesema uwepo wa mradi huo utasaidia  kuondoa migogoro ya ardhi   hivyo ni vyema utekelezaji wake ukafanyika kwa umakini.

Naye Mratibu wa Mradi huo Bw Godfrey Machabe amesema mradi huo umeanza japo unakutana na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi lakini wanafanya kila liwezekanalo kuhakisha kuwa wanafikia lengo lilokusudiwa.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walipata nafasi ya kuhoji mambo mbalimbali kuhusu mradi na kupatiwa majibu na  viongozi.

0 Responses to “WAZIRI LUKUVI AZITAKA HALMASHAURI KUWASILISHA ORODHA YA MASHAMBA PORI AMBAYO HAYAJAENDELEZWA.”

Post a Comment

More to Read