Thursday, June 16, 2016

JE NI KILIO NA MWISHO WA TAX TANZANIA ..?





Kwa kuanzia na jiji la Dares Salaam kampuni ya Uber Tanzania limited, imetambulisha rasmi matumizi ya Tax za ambazo pamoja na kuwa na gharama nafuu zaidi Tsh 466 kwa kilometa, wateja wake watapa nafasi ya kuweza kufanya booking za Tax  kwa kutumia program ya Simu iitwajo Uber (Uber App), mteja kuweza kulipa kwa kutumia njia ya M-pesa kwa wateja wote wa Vodacom.

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uber katika ukanda wa jangwa la Sahara Afrika Mr. Alon Lits alisema “ kampuni ya Uber inampa mteja njia mahususi ambayo inamwunganisha yeye pamoja na dereva katika wakati husika”.

“Dar es Salaam ni jiji la 9 kuunganishwa na mfumo wa Tax za Uber katika bara la Afrika baada ya nchi ya Uganda na Ghana kujiungana mfumo huu wiki iliyopita, Dar es Salaam inakuwa ni jiji la 475 kuunganishwa katika huo  duniani ambapo kwa sasa mfumo huu unafanya kazi kwa zaidi ya nchi 70”.  
Aliongeza Mr. Lits

Meneja wa Uber Tanzania Mr. Alfred Masemo alisema pamoja na uhakika wa kupata bei nafuu katika Tax za Uber, Uber inahakikisha Usalama situ wa mteja bali pamoja na dereva.

“Hata rafiki yako anaweza kufuatilia ni wapi na jinsi gani Tax inakwenda kwa wakati husika bila hata kulazimika ku-download program ya Uber (Uber App) kwenye simu yake na hii ni kwa kutumia GPS (mfumo unaokuwezesha kujua mahali, muda na taarifa za hali ya hewa za sehemu husika). Na kitu chochchote kikitokea kwa gari au ajali au kitu kingine chochote ambacho hakikutarajiwa, wafanyakazi wetu kwenye kitengo cha Huduma kwa wateja watalifanyia kazi muda huo huo”.
Alisema Mr. Alfred

Uber Tanzania imeungana na benki ya FNB pamoja na kampuni ya Vodacom kwa ajili ya kuhakikisha shughuli zote baina ya mteja na dereva zinakwenda salama.

0 Responses to “JE NI KILIO NA MWISHO WA TAX TANZANIA ..?”

Post a Comment

More to Read