Thursday, June 16, 2016
IKIWA LEO NI SIKU YA MTOTO WA AFRKA MATUKIO YA UBAKAJI WA WATOTO YAFIKIA 2358 KWA MWAKA
Do you like this story?
MATUKIO ya ubakaji
watoto yameongezeka hadi kufikia 2358 kwa mwaka 2015 ikilinganishwa na 422 ya
mwaka 2014 na kufanya vitendo hivyo kuwa tishio kwa watoto nchini.
Hayo yalibainishwa
jana mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
“Asilimia 49 ya
unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto hufanyika majumbani, wakati asilimia 23
hufanyika njiani wakati wa kwenda au kutoka shule na asilimia 15 hufanyika
shuleni,”alisema Ummy.
Akionyesha
kusikitishwa na ongezeko hilo la vitendo viovu dhidi yawatoto, Ummy alisema
kuwa hali hii inatisha na kukera kwani ndani ya miezi mitatu mwaka huu yaani
januari hadi Machi 2016 matukio 1765 yameripotiwa katika vituo mbalimbali vya
polisi.
Aidha, Ummy alisema
kuwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifali
linaloshughulikia masuala ya watoto (UNICEF) ilifanya utafiti kuangalia hali
halisi ya Ukatili dhidi yawatoto na kubaini kuwa wasichana 3 kati 10 na mvulana
mmoja kati ya 7, wamefanyiwa ukatili wa kingono angalau mara kabla ya kutimiza
miaka 18.
Kwa mujibu wa Wazirti
Ummy alisema Utafiti huo pia umeonyesha kuwa wasichana 4 kati ya 10
na wavulana 3 kati ya 10 wamefanyiwa ukatili zaidi ya mara tatu kabla ya
kufikisha miaka 18, na wasichana 6 kati ya 10 wamefanyiwa ukatili ndani ya
familia zao na msichana mmoja hadi wawili wamefanyiwa na walimu wao.
“Msikubali kuwalaza
chumba kimoja watoto wa kike na ndugu wa kiume kwani tabia hizo chafu zimekuwa
zikifanywa na watu wa familia,” alisema Ummy.
Aliongeza kuwa
vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto vina athari kubwa sana katika
ustawi wa watoto.
Aidha alisema kuwa
Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kisera na kisheria katika
kusimamia utekelezaji wa haki ya motto ya kuishi, kulindwa na kuendelezwa,
ikiwemo na kufanya mabadiliko ya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inayohalalisha
motto wa miaka 15 kuolewa kwa ridhaa ya wazazi na wa miaka 14 kwa kibali cha
mahakama,” alisema Ummy.
Alisisitiza kuwa
muswada wa Sheria ya Ndoa inabidi uletwe bungeni haraka iwezekanavyo na
kuongeza kuwa mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria hiyo yameshapelekwa katika
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Imeandaliwa na Jonas
Kamaleki Maelezo, Dodoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “IKIWA LEO NI SIKU YA MTOTO WA AFRKA MATUKIO YA UBAKAJI WA WATOTO YAFIKIA 2358 KWA MWAKA”
Post a Comment