Thursday, June 16, 2016
SERIKALI KUTUNGA SHERIA KUPIGA MARUFUKU WASICHANA WA KAZI CHINI YA MIAKA 18
Do you like this story?
SERIKALI
imekusudia kutunga sheria ya kupiga marufuku ajira za wasichana wa kazi wenye
umri chini ya miaka 18 kabla ya mwisho wa mwaka 2016.
Hatua hiyo
inaelezwa inakusudia kuinua hadhi ya kazi na ajira za wasichana wa kazi
nchini, kwani muda wa kurasimisha ajira hizo umefikia wakati wake.
Hayo
yamebainishwa jana mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumzia na waandishi wa habari
kuhusu maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika inayoadhimishwa tarehe 16 Juni
kila mwaka.
Alisema
hatua inachuliiwa na Serikali kutokana na wasichana wengi wa ndani
kutumikishwa kazi hiyo katika umri mdogo na kulipwa ujira mdogo.
“Tumepanga
kutunga kanuni na sheria ya kupiga marufuku ajira za wasichana wa kazi wenye
umri chini ya miaka 18, na ndio maana tunawachukua katika umri mdogo sana na
kuwalipa ujira mdogo, hivyo ukimchukua binti wa miaka 18 utaweza kuinua hadhi
ya kazi ya kazi yenyewe” alisema
Waziri Ummy.
Akizungumzia
kuhusu maadhimisho hayo, Waziri Ummy aliitaka jamii kukataa kurubuniwa kwa pesa
na katika kuwafichua watu wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo
kulawiti na kuwabaka na badala yake watoe taarifa katika vyombo vya dola ili
adhabu kali zichuliwe dhidi yao.
Aidha
Waziri Ummy aliwata wazazi nchini kujenga tabia ya kukagua maumbile ya watoto
wao hususani watoto wa kike ikiwemo kuwaogesha angalau mara moja kwa mwezi,
kwani kwa kufanya hivyo kutamwezesha mzazi kufahamu afya ya kimwili ya motto
wake.
Kwa mujibu
wa Waziri huyo alisema vitendo vya ulawiti havifanywi kwa watoto wa kike pekee
bali na watoto wa kiume pia wamekuwa wahanga wa vitendo hivyo, ambapo ameitaka
jamii kutowaamini ndugu au jamaa zao kulala kitanda chumba kimoja na watoto
wao.
“Kwa
mujibu wa taarifa za jeshi la Polisi, vitendo hivi vimekuwa vikifanyika zaidi
majumbani kwa asilimia 49, asilimia 23 wakati wa kurudi na kwenda shule
na asilimia 15 wakiwa shuleni, hivyo kwa takwimu hizi unaweza kuona ukubwa wa
tatizo ulivyo” alisema Waziri Ummy.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI KUTUNGA SHERIA KUPIGA MARUFUKU WASICHANA WA KAZI CHINI YA MIAKA 18”
Post a Comment