Tuesday, June 14, 2016
POLISI WASIOWAPIGIA SALUTI WABUNGE KUKATWA MSHAHARA.
Do you like this story?
Mbunge wa
Viti Maalumu (CCM), Fakharia Khamis amehoji bungeni adhabu gani askari anapewa
ikiwa atashindwa kutoa saluti kwa mbunge.
Katika
swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua maana ya saluti kwa askari ni nini,
na viongozi gani wa uraiani wanaotakiwa kupigiwa saluti katika mhimili wa
Bunge, Serikali na Mahakama.
Akijibu
swali la mbunge huyo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole
Nasha kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alisema Serikali imetangaza
adhabu ya kuwakata mishahara na adhabu nyingine, askari polisi wote nchini
ambao hawatawapigia saluti wabunge wa Bunge la Muungano na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Ole Nasha
alisema kumpigia saluti mbunge ni jambo la lazima kwa askari kwa kuwa lipo
kwenye moja ya masharti yao, hivyo kutokufanya hivyo ni kushindwa kutii kiapo
cha uaminifu wao.
“Askari
asipotoa saluti unatakiwa kumripoti kwa kiongozi wake ambapo atapewa adhabu
ikiwamo kukatwa mshahara, kupigishwa paredi, kufanya usafi katika maeneo ya
vituo na adhabu nyingine nyingi zinazofanana na hizo,” alisema Ole Nasha.
Alisema
saluti ni salamu ya kijeshi ambayo hutolewa na askari kwa mujibu wa kanuni za
kudumu za utendaji za jeshi la polisi (Police General Orders –PGO No 102).
Naibu
Waziri alisema sheria hiyo imewataja askari wa vyeo vyote kuwa wanatakiwa
kupiga saluti kwa Rais wa Jamhuri na Rais wa Zanzibar, Makamu wa Rais na Makamu
wawili wote wa Zanzibar, majaji wakuu wa Muungano na Zanzibar.
Wengine ni
Spika wa Muungano na Zanzibar, mawaziri wote wa Jamhuri na Zanzibar, makatibu
wa Bunge na Baraza la Wawakilishi, wabunge wa muungano na wawakilishi
wanapokuwa kwenye maeneo yao, wakuu wa mikoa, majaji wanapokuwa kwenye maeneo
yao na kwa nafasi zingine ni wakuu wa wilaya na mahakimu kwenye maeneo yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ POLISI WASIOWAPIGIA SALUTI WABUNGE KUKATWA MSHAHARA.”
Post a Comment