Monday, June 13, 2016

UVCCM MKOA WA MBEYA & SONGWE KUMPONGEZA MHE. DR. TULIA ACKSON MWANSASU (MB) NAIBU SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


Mwenyekiti wa Vijana Uvccm Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna akitoa tamko kwa Wanahabari katika ofisi za Mkoa ccm.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Mwenyekiti wa Uvccm Wilaya Maranyingi Matukuta akisisitiza Msimamo wake.




TAMKO LA UVCCM MKOA WA MBEYA & SONGWE  KUMPONGEZA MHE. DR.  TULIA  ACKSON
MWANSASU (MB) NAIBU SPIKA WA BUNGE
LA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA 13/6/2016.
Ndugu wana habari na watanzania mnao tufuatilia kupitia redio na televisheni tupo hapa mbele yenu kwa lengo mahususi la kumpongeza Mhe. Dr. Tulia Ackson Mwansasu (MB) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa kazi nzuri anayo ifanya katika kuliongoza na kulisimamia Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa umahiri na ueledi na wa hali ya juu.

Watanzania wote ni mashahidi kwa namna ambavyo Mhe. Dr. Tulia Mwansasu anavyo lisimamia na kuliongoza Bunge letu kwa kuzingatia sheria, kanuni, na maadili ya Bunge na hivyo kurejesha heshima, nidhamu na uwajibikaji kwa Wabunge katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwawakilisha wananchi.

Kwa mfano hivi  karibu tumeshuhudia akitoa mwongozo wa kutokulipwa fedha Wabunge wanaoingia Bungeni na kutoka mara tu baada ya kujisajili pasipo kutimiza wajibu wao hasa kwa kuzingatia kuwa HAKI na WAJIBU vinakwenda pamoja.

Vile vile  kipekee kabisa na kwa umuhimu mkubwa UVCCM Mkoa wa Mbeya & Songwe tunapenda kumshukuru Mhe. Rais wetu  Mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa kumteua Mhe. Dr, Tulia Mwansasu (MB) kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kisha kuteuliwa na CHAMA CHA MAPINDUZI kuwa Mgombea pekee wa nafasi ya Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye  kuaminiwa kwa kuchaguliwa na Waheshimiwa Wabunge wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura nyingi na za kishindo.

Sanjali na hivyo tunapenda kumpongeza Mhe. Rais wetu Mpendwa Dr. John  Pombe Magufuli kwa  hatua mbali mbali anazo endelea kuzichukua katika kutuletea Maendeleo Wananchi wa Tanzania ikiwa  ni pamoja na kupiga vita rushwa kwa vitendo. 

Pia tunawashukuru na kuwapongeza sana Waheshimiwa wabunge wote wanao tokana na CHAMA CHA MAPINDUZI Kwa Kazi kubwa wanayo endelea kuifanya katika kuisimamia na kuishauri  serikali ,UVCCM Mbeya & Songwe tunawashukuru sana kwa namna ya kipekee wanavyo endelea kumpatia ushirikiano wa kutosha Mhe. Rais wetu mpendwa na Mhe, Naibu Spika wetu Mungu awabariki.

Tunasikitishwa na kulaani vikali vitendo vinavyo fanywa na Wabunge wa Upinzani vya kutaka KUMHUJUMU Mhe, Naibu Spika kwa sababu zao binafsi zisizo na maslahi kwa Umma isipo kuwa kwa vyama vyao pekee kwani huwezi kumuundoa Mhe, Naibu Spika kwa kusimamia kanuni na taratibu zilizo tungwa na wao wenyewe waheshimiwa Wabunge na kuwanyima wananchi walio wachagua haki yao ya msingi ya kuwawakilisha kwa kususia vikao vya Bunge kwa kisingizio cha kutokuwa na IMANI na Naibu Spika ili hali lengo lao ni kuhakikisha wanapata nafasi ya kuendeleza mizaha na siasa zisizo na tija kwa Taifa letu ndani ya Bunge kwani nidhahiri kuwa hivi sasa Wapinzani wamekosa Ajenda za kuzisimamia baada ya vyama vyao kuwakaribisha na kuwakumbatia Mafisadi pia kwa kazi nzuri inayofanywa na Mhe, Rais ya kutatua kero za Wananchi kwa kiwango kikubwa. Na zaidi sifa, uwezo na uweledi alionao Mhe, Naibu Spika Dr. Tulia Ackson Mwansasu vinavyomuwezesha kulisimamia na kuliongoza Bunge  kikamilifu ikumbukwe Mhe, Dr, Tulia Ackson Mwansasu ni msomi na mbobezi wa sheria kwa kuzisoma, kuzifundisha, kuziandika na kuzifanyia kazi hivyo Mhe, Naibu Spika anachokifanya ni kuzisimamia na kuzitekeleza sheria na kanuni za Bunge zilizotungwa na Bunge na hakuna kanuni mpya alizokuja nazo Mhe, Naibu Spika, kama Wapinzani wanavyotaka kuwaaminisha Wananchi.

UVCCM Mbeya & Songwe tunasema Usirudi nyuma Mhe. Dr. Tulia Ackson Mwansasu watanzania wengi tupo nyuma ya kazi yako njema na yenye maslahi kwa Taifa.

RAI YETU KWA WAPINZANI
Tunawashauri Ndugu zetu wa upinzani kurejelea maneno ya busara tuliyo kumbushwa hivi karibuni na Waziri wa sheria na katiba Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe (MB) kutoka kwa Mwana falsafa nguli wa Ugiriki “PLATO”  aliye pata kusema “wenye busara husema wanapokuwa na kitu cha kusema,  wapumbavu husema ili mradi waseme chochote”. Ni dhahiri kwamba Wapinzani hawana cha kuwaambia Watanzania kwa muda huu hivyo sio  muda muafaka kwao kutaka kuzunguka nchi nzima kuwahadaa wananchi. Hata hivyo upinzani wanatakiwa kulishukuru sana jeshi la Polisi kwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa kwani kwa kufanya hivyo limewaondolea aibu kubwa  ambayo wangeipata kwenye Ziara yao kwa kupuuzwa na wananchi.

Tunawataka wabunge wa upinzani warejee Bungeni kuwawakilisha wananchi walio wachagua kwa kuwatetea kwa hoja za msingi zenye maslahi kwa Taifa na sio vyama vyao pekee.

Vivyo hivyo tunawaomba upinzani kubadilisha matumizi ya fedha walizokuwa wamepanga kuzitumia kuzunguka nchi nzima, badala yake wazipeleke kwenye ununuzi wa Madawati kwenye majimbo yao ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli  katika kukabiliana na uhaba wa Madawati nchini.

Mwisho japo sio kwa umuhimu UVCCM Mkoa wa Mbeya na Songwe tunawatakia  waislam wote wa  Tanzania mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na tunawaomba watanzania wote tuwape ushirikiano Ndugu zetu katika wakati huu muhimu kwa kutenda matendo mema yampendezayo Mwenyezi Mungu.

MUNGU IBARIKI MBEYA NA SONGWE, MUNGU MBARIKI MHE. DR. TULIA ACKSON MWANSASU MUNGU IBARIKI TANZANIA Asanteni kwa kutusikiliza.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na
Amani L Kajuna
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya & Songwe

0 Responses to “UVCCM MKOA WA MBEYA & SONGWE KUMPONGEZA MHE. DR. TULIA ACKSON MWANSASU (MB) NAIBU SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA”

Post a Comment

More to Read