Monday, June 13, 2016
JPM AWAAPISHA MWIGULU NCHEMBA NA TIZEBA.
Do you like this story?
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
leo amewaapisha Mh. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
kuchukuwa nafasi ya Dkt. Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwana
huku Injinia Dkt. Charles Tizeba akiapishwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kuapishwa, Mh. Mwigulu Nchemba ametoa agizo la kuwataka
wafanyabiashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara
hiyo badala yake watafute shughuli halali za kujiingizia kipato.
Aidha
Waziri Nchemba alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama wa Raia
na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na utulivu katika nchi.
Naye
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa atahakikisha
anashirikiana na wataalum wa sekta tatu zilizo katika Wizara yake ili kufanya
mapinduzi katika maeneo hayo yaliyoajiri zaidi ya asiimia 80 ya Watanzania.
Pia Waziri
Dkt. Tizeba alisema kuwa Wizara itahakikisha inashugahulikia changamoto zinazozokabili
vyama vya ushirika ambavyo vimekuwa havifanyi vizuri katika miaka ya hivi
karibuni.
Mawaziri
walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt.
Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba
aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayejaza nafasi iliyoachwa wazi
baada ya Rais kutengua uteuzi wa Mh. Charles Kitwanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JPM AWAAPISHA MWIGULU NCHEMBA NA TIZEBA.”
Post a Comment