Monday, July 4, 2016
BWAWA NYUMBA YA MUNGU LAFUNGIWA KWA MIEZI 12
Do you like this story?
SERIKALI
za mikoa ya Kilimanjaro na Manyara zimelifunga Bwawa la Nyumba ya Mungu kwa
kipindi cha mwaka mmoja ili kuepusha kutoweka kwa viumbe hai wakiwamo samaki
kutokana na kushamiri kwa uvuvi haramu.
Aidha, wakuu
wa wilaya za Moshi, Mwanga na Simanjiro wametakiwa kusimamia maamuzi hayo na
kuchukua hatua kali za kisheria kwa watakaokaidi agizo hilo.
Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadiki alisema hayo wakati wa hafla maalumu ya
kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya mkoani Kilimanjaro iliyofanyika mjini Moshi,
juzi.
Alisema
uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha ujirani mwema baina ya mikoa hiyo kupitia
wilaya tatu zinazolizunguka bwawa hilo na kwamba utekelezaji wa agizo hilo
umeanza rasmi Julai Mosi mwaka huu.
“Hali
ya uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ni mbaya sana, mazingira
yameharibiwa, kuna athari nyingi zinajitokeza ikiwamo ya kupungua kwa maji
katika bwawa hilo na hii huenda ikaathiri uzalishaji umeme na kutoweka kwa
viumbe hai....kama serikali hatuwezi kuvumilia tena,” alisema Sadiki.
Pamoja na
bwawa hilo, Sadiki alitaka wakuu wa wilaya kusimamia agizo la Kamati ya Ushauri
ya Mkoa (RCC), kupiga marufuku misumeno ya mnyororo, kwani imebaini ni adui
mkubwa wa misitu.
Katika
hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa aliwakabidhi wakuu hao wa wilaya migogoro
mikubwa mitano iliyopo katika hatua mbalimbali za utatuzi wake kupitia viongozi
waliowatangulia na kutaka kufuata sheria katika kuishughulikia.
Miongoni
mwa migogoro aliyoitaja ni unaohusisha jamii ya wafugaji wanaozunguka Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kampuni inayohudumia uwanja huo ya
KADCO kuhusu umiliki wa eneo la ardhi.
Mgogoro
mwingine ni wananchi wa wilaya ya Longido mkoani Arusha na mwekezaji wa eneo la
utalii la Ndarakwai uliowahi kusababisha kuchomwa moto kwa eneo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BWAWA NYUMBA YA MUNGU LAFUNGIWA KWA MIEZI 12”
Post a Comment