Wednesday, August 17, 2016
AZAM WAVUNJA MWIKO WA NGAO YA JAMII, WAITWANGA YANGA KWA MATUTA.
Do you like this story?
AZAM
FC wameibuka washindi na kutwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza kufuatia
kuifunga Yanga kwa changamoto za mikwaju ya penati 4-1, baada ya kumaliza
dakika tisini kwa sare ya mabao 2-2, mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.
Ndani
ya dakika tisini, Yanga walianza kupata mabao yao kupitia kwa Mzimbabwe Donald
Ngoma kwa njia ya penati na Amissi Tambwe, huku Azam wakisawazisha kupitia kwa
beki wa kulia Shomari Kapombe na John Bocco kwa njia ya penati.
Ulipowadia
wakati wa mikwaju ya penati, Azam walipata penati zao zote zilizopigwa na John
Bocco, Himid Mao, Shomari Kapombe na Kipre Balou, huku Yanga wakipata moja
iliyopigwa na kipa Deogratius Munishi wakati Haruna Niyonzima na Hassan Kessy
wakikosa.
Yanga;
Deogratius Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji Mngwali, Mbuyu Twite,
Vincent Bossou, Said Juma ‘Makapu’, Haruna Niyonzima, Juma Mahadhi/Malimi
Busungu dk81, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Simon Msuva dk67 dk na Donald
Ngoma.
Azam;
Aishi Manula, Isamil Adam, Bruce Kangwa, David Mwantika, Himid Mao, Jean
Baptiste Mugiraneza, Shomary Kapombe, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Kipre Balou
dk90, John Bocco, Shaaban Chilunda/Mudathir Yahya dk46 na Ramadhani Singano
‘Messi’/Francesco Zekumbariwa dk46.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AZAM WAVUNJA MWIKO WA NGAO YA JAMII, WAITWANGA YANGA KWA MATUTA.”
Post a Comment