Wednesday, August 17, 2016
WAKUU WA SHULE ZA MSINGI 68 KUVULIWA VYEO VYAO JIJINI DAR ES SALAAM.
Do you like this story?
WALIMU
wakuu wa shule 68 wa shule za Msingi wanatakiwa kuvuliwa na kunyang'anywa
vyeo vyao kwa kosa la udananyifu wa takwimu za wanafunzi hewa tangu elimu
itangazwe kuwa bure.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Amesema
kuwa walimu wakuu hao wametakiwa kuvuliwa vyeo vyao na kuwapa walimu wengine
kwa kosa la kutoa takwimu za wanafunzi hewa 3462 wa shule za msingi 68 za
Wilaya ya Kinondoni. Pia hatua kali za Kisheria zitachukuliwa kwa dhidi ya
walimu wakuu wa shule hizo.
Pia
Hapi amemwomba Katibu Tawala wa Mkoa kuwavua vyeo wakuu wa shule 22 wa shule za
Sekondari 22 za Manispaa ya Kinondoni na Ubungo kwa kosa la kutoa takwimu za
uongo na kuweka wanafunzi hewa.
Wakuu
wa shule za Msingi hao wamekuwa na wanafunzi hewa 2534 kutoka shule 22 za
Sekondari za Manispaa ya Kinondoni na Manispaa ya Ubungo.
Wakuu
wa shule hizo wameisababishia Serikali kupoteza zaidi ya shilingi milioni 60
kwa kupeleka fedha za kuwahudumia wanafunzi wanaosoma katika shule hizo.
Baadhi
ya shule za sekondari zilizokutwa na wanafunzi hewa ni Boko wanafunzi 74, Bunju
B155, Goba Mpakani 42 na Hananansifu wanafunzi 154. Na shule za Sekondari ni
Msisiri B wanafunzi hewa 395, Upendo 273 na Ubungo Msewe 267.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAKUU WA SHULE ZA MSINGI 68 KUVULIWA VYEO VYAO JIJINI DAR ES SALAAM.”
Post a Comment