Thursday, August 18, 2016
NDALICHAKO ATOA SIKU SABA KWA VYUO VIKUU KUREJESHA FEDHA ZISIZOSTAHILI
Do you like this story?
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ametoa siku saba kwa vyuo vikuu vilivyopokea
fedha za wanafunzi ambao hawapo vyuoni kwa mwaka wa 2015/16 kuzirejesha
wizarani mara moja.
Taarifa hiyo ameitoa mbele ya maafisa kutoka wizarani mwake,
pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo, na Mchunguzi Mkuu wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru na wengineo.
Kwa mujibu wa Waziri Ndalichako,
uhakiki huo umefanywa na watumishi wa bodi ya mikopo kwa kushirikiana na
TAKUKURU kati ya mwezi Mei hadi Julai mwaka huu ambapo wanafunzi wanufaika wa
mikopo walitakiwa kujitokeza na kuonana na jopo la uhakiki ili kutambuliwa na
kuhakikiwa.
Jumla ya vyuo vya elimu ya juu nchini
Tanzania 31 kati ya 81 ndivyo vilivyohakikiwa. Zoezi hilo la uhakiki limefanywa
katika awamu tatu kwa kila taasisi ili kuwapa nafasi wanafunzi ambao hawakuweza
kujitokeza kwa uhakiki awamu ya kwanza,kujitokeza katika awamu zilizofuata.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NDALICHAKO ATOA SIKU SABA KWA VYUO VIKUU KUREJESHA FEDHA ZISIZOSTAHILI”
Post a Comment