Wednesday, August 17, 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA AWATEMBELEA WAHANGA WA KUPISHA HIFADHI RUAHA






MKUU WA MKOA wa Mbeya Amos Makalla Leo amefanya ziara ya kikazi kata ya MADIBIRA wilaya ya mbarali na kuongea na wahanga waliopisha hifadhi ya Ruaha tangu mwaka 2008 wamekuwa wakufuatilia malipo YA nyongeza YA fidia baada ya fidia waliolipwa kuwa na upungufu 

Akiwa katika mkutano wa hadhara kijiji cha Ikonga mpya amewahaidi kuwa serikali kupitia Tanapa kabla mwezi huu haujaisha watalipa mapunjo YA Fidia sh miloni 362 kwa wananchi wote wanastahili vikwazo mujibu wa sheria hivyo amewaomba wawe watulivu wakati yeye anafuatilia malipo hayo

Aidha ametangaza Mbele YA mkutano ubadhirifu wa Fedha za fidia sh milioni 192 zilivyoliwa na watendaji wa halmashauri ya Mbarali wakati zoezi la kulipa fidia lilipofanyika mwaka 2007
Kwa mujibu wa Mkuu wa MKOA baada ya kutokea malalamiko ofisi yake ilimuomba CAG afanye ukaguzi maalum ambapo Matokeo yameinyesha jumla YA sh milioni 192 zimetafunwa kwa mchanganuo sh 156,523,000 zilizokuwa zijenge Shule na zahanati katika makazi mapya hazionekani, Fedha sh 26,393,000 zimelipwa kwa mdai hewa na sh 9,609,000 zilizokuwa fidia kwa ajili ya msikiti kijiji cha Msangaji nazo hazionekani

Kufuatia taarifa hiyo pamoja na watendaji wote waliohusika wamehama wilaya ya Mbarali ameagiza watafutwe popote walipo kuja kujibu mashtaka ikiwemo kurejesha Fedha na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao

Aidha amemwagiza mkurugenzi wa mbarali kutafuta fedha na kuzipeleka kwa wananchi kujengewa Shule na zahanati kama ilivyokusudiwa " Hapa nisisitize hela hizi zimepotelea kwenye dhamana yenu ila haki YA wananchi ipo palepale toeni hela za halmashauri wajengewe shuke na zahanati nyie watafuteni waliokula hizo hela wazirudishe "

Amewahakikishia wananchi kuwa serikali YA MKOA itafuatilia kwa Karibu utekelezaji wa maagizo hayo na kuwaomba ushirikiano katika kushughulikia mapunjo ya fidia.

0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA AWATEMBELEA WAHANGA WA KUPISHA HIFADHI RUAHA ”

Post a Comment

More to Read