Wednesday, August 17, 2016
KAMISHNA WA TRA AZINDUA KAMPENI YA UHAKIKI WA NAMBA YA MLIPA KODI (TIN)
Do you like this story?
Mamlaka
ya Mapato Tanzania TRA imewataka wafanyabiashara katika jiji la Dar es salaam
kuboresha taarifa za usajili wa namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ili
kuondokana na mfumo wa kizamani wa usajili wa namba hiyo.
Uhakiki
huo utaiwezesha mamlaka hiyo kuweza kujua idadi sahihi ya wafanyabiashara
walipa kodi, kuondoa walipa kodi hewa ambao wamekuwa hawajihusishi na biashara
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo au kufungwa kwa makampuni yao.
Akiongea
na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania ndugu Alphayo Kidata alisema mfumo huo utawawezesha
wafanyabiashara kulipa kodi kwa gharama nafuu sambamba na kuweka mazingira ya
ulipaji kodi kwa hiari.
Kidata
alisema kuwa mfumo wa sasa wa uhifadhi kumbukumbu za walipa kodi ulikuwa na
kasoro nyingi hivyo mfumo mpya utaendana na ukuaji wa teknolojia na kukuza
uchumi.
“Zoezi
hili linamtaka kila mwenye namba ya utambulisho yani TIN kufika katika ofisi za
TRA zilizopo karibu naye bila kuwakilishwa na mtu yeyote na zoezi litatumia
dakika 10 kumalizika” alisema
Naye
Elija Mwandubya ambaye ni kamisha wa mapato wa ndani wa mamlaka hiyo, alisema
zoezi hilo litachukua siku 60 na kuanzia Dar es salaam na baadaye kuhamia mikoa
mingine ndani ya nchi.
“TRA
ina wafanyabiashara walipa kodi milioni mbili na laki moja hivyo uboreshwaji wa
TIN utatupa uelewa wa idadi kamili ya walipa kodi” Alisema
Elija
alisema kutakuwa na vituo maalum kwaajili ya uhakiki wa taarifa katika mikoa ya
kikodi ambapo Kinondoni wafanyabiashara watatakiwa kutembelea ofisi za TRA
zilizopo jengo la LAPF – Kijitonyama na Kibo Complex Tegeta.
Ilala
wafanyabiashara watembelee ofisi ya TRA shauri moyo na 14 Rays Gerezani na
Temeke wafike ofisi za uwanja wa Taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KAMISHNA WA TRA AZINDUA KAMPENI YA UHAKIKI WA NAMBA YA MLIPA KODI (TIN)”
Post a Comment