Friday, October 21, 2016

MOUNTAIN RANGE MBEYA KUWA ENEO LA MAZINGIRA NYETI:JANUARY MAKAMBA




Mhe. January Makamba, Waziri wa Mazingira na Muungano ofisi ya Makamu wa Rais akifafanua jambo kwa Viongozi mbalimbali waliochini ya Wizara yake.




Mhe. January Makamba, Waziri wa Mazingira na Muungano ofisi ya Makamu wa Rais  ametangaza eneo la Mbeya Mountain Range kua ni eneo la ‘MAZINGIRA NYETI/ENVIRONMENTALLY SENSITIVE AREA". Wiki ijayo uamuzi huu utapelekwa kutangazwa kwenye ‘Government Gazette” kupelekea usimamizi wake kuanza rasmi. Agizo hili la Mheshimiwa January Makamba amelitoa kwa kuzingatia kifungu cha Sheria ya Usimamizi ya Mazingira ya Mwaka 2004. 

Ametumia kifungu N0. 51 Kinachosema; 1. Pale Waziri atakapoona inabidi, anaweza kutangaza kwa amri itakayotangazwa kwenye Gazetli la Serikali, eneo lolote kuwa mazingira nyeti kwa mujibu wa Sheria hii. 

2. Usimamizi wa eneo la mazingira nyeti kwa mujibu wa fungu hili utafanywa kwa kuzingatia taratibu zitakazotolewa na waziri.
3. Mtu yeyote atakayeshindwa, kupuuza au kukataa kuzingatia taratibu zilizobainishwa kwatika kusimamia maeneo ya mazingira nyeti atakuwa anatenda kosa.

 Eneo la Mbeya Range Mountains limekua likiathirika kwa ukataji miti hovyo pamoja na ukataji unaofanywa ki biashara kwa ajili ya mahitaji mbali mbali ya miti ikiwa ni pamoja na nguzo za umeme unaofanywa na Tanzania Forestry Services (TFS) pamoja na wafanyabiashara wa mkaa. Eneo hili kuingizwa kwenye Mazingira Nyeti ni hatua nzuri na ya lazima. Mheshimiwa January Makamba alisema “ Nimefanya maamuzi haya kwasababu vyanzo vya maji yanayokuja Mbeya yanatokea huko lakini watu wameshindwa kabisa kudhibiti uharibifu wa vyanzo hivyo. 

Miaka ya nyuma kulikuwa na vyanzo 49 lakini sasa vimebakia 4. Tangazo hili litawezesha zuio la kisheria la matumizi ya kibinadamu katika milima hiyo, ikiwemo uvunaji wa miti unaofanywa na Mamlaka ya Misitu TANZANIA (TFS).

 Vilevile naelekeza milima hiyo kuanza kupandwa kwa miti ya asili inayohifadhi maji”. Hii ni mara ya kwanza kifungu hiki cha Sheria hii kinatumika.

 Waziri Makamba aliongeza na kusema “Hapa ndio eneo la kwanza, lakini tuna nia ya kutangaza mengine mengi zaidi”. Mbeya Mjini kwasasa inahitaji lita milioni 50 za maji kwa siku, kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji katika safu za Milima ya Mbeya, ifikapo mwaka 2018, maji katika mji wa Mbeya hayatawatosha wakazi wa Mbeya. 

Hatua hii haina budi kupongezwa, wakazi wa Mbeya mna kila sababu ya kushiriki kusimamia agizo hili na kuisaidia serikali katika azma yake ya kulinda mazingira kwa manufaa yetu na ya vizazi vijavo. 

Waziri January Makamba alianza ziara yake tarehe 16/Oktoba/2016 ya kutembelea mikoa 10 ya Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora na Dodoma. Mikoa hii imeathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi na kuporomoka kwa hifadhi za mazingira kwa ujumla nchini. Waziri January Makamba anaendelea na ziara Mbeya leo, anatazamiwa kwenda Ofisi za NGO za mazingira za Kimataifa World Conservation Society (WCS) na Africa Wildlife Fund (AWF).

1 Responses to “MOUNTAIN RANGE MBEYA KUWA ENEO LA MAZINGIRA NYETI:JANUARY MAKAMBA”

Unknown said...
October 22, 2016 at 3:07 PM

nimekerwa na uharibifu unaofanyika maana watu wameruhusiwa kujenga mpaka karibu na vyanzo vya maji hasa juu ya mlima Loleza watu wanazidi kujenga nyumba za kuish ilihali chini ndiko kuna vyanzo vya maji ambavyo ndivyo vinavyotiriruisha maji jijini, hii ilinifanya nifikiri kuwa kama viongozi wa mkoa na wilaya hawajaliona je wasimamizi wa mazingira wako wapi? ningeomba wananchi waliojenga juu ya mlima loleza karibu na Iziwa wapewe eneo lingine wajenge ili yale maeneo yapandwe miti na yako maeneo mengine ya wazi ambayo miti ikipandwa itasaidia kuupendezesha mji na kutunza mazingira kiujumla


Post a Comment

More to Read