Tuesday, November 1, 2016
JELA MWAKA MMOJA KUMDHALILISHA MAMA YAKE MZAZI
Do you like this story?
Mwanaume
mkazi wa Ilala, Siwema Seif (40) amehukumiwa na Mahakama ya Mwanzo ya Ilala
kwenda jela mwaka mmoja kwa kumtolea lugha ya matusi na kumdhalilisha kimwili,
Zainab Ramadhan ambaye ni mama yake mzazi.
Akisoma
hukumu mahakamani hapo jana, Hakimu wa Mahakama hiyo, Matrona Luanda alisema
ushahidi uliotolewa na shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji, ulionesha
kukosa shaka na kumtia hatiani mshitakiwa.
Shahidi
huyo alisema siku ya tukio mshitakiwa alifika nyumbani kwao akaomba chakula
akajibiwa kuwa kuna wali na mshitakiwa akasema hataki wali bali anataka ugali
na mama akamjibu asingeweza kupika ugali na kumsisitiza Siwema ale wali.
Zainab
alisema baada ya majibizano hayo, mshitakiwa alimtukana matusi ya nguoni mama
yake, huku akisema hawezi kumzaa na kumkashifu, kwamba hana sehemu ya kumzalia
huku akitishia kumwua akiahidi kumtoa roho ndipo amjue yeye ni nani.
Kwa
mujibu wa Zainab, alipoona ugomvi na matusi umezidi aliingia chumbani mwake, na
ndipo mlalamikaji akamfuata na kumtukana huku akitishia kumwingilia kinyume cha
maumbile.
“Baada
ya hapo mshitakiwa alinivamia na kunidhalilisha kimaumbile kwa mikono yake,” alisema.
Baada
ya ushahidi wa mama huyo dhidi ya Siwema, Mahakama ilitoa nafasi kwa kijana
huyo kujitetea na Mahakama ikamtia hatiani.
Karani
wa mahakama hiyo, Blanka Shao alisema kwa kuwa mshitakiwa alikuwa mkosaji wa
mara ya kwanza na kitendo alichokifanya ni cha kifedhuli tena haonyeshi
kujutia, alishauri apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake.
Hakimu
Luanda alimhukumu kwenda jela mwaka mmoja kwa kitendo alichomfanya mama yake
mzazi.
Awali,
ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 9 Ilala,
mtaa wa Sophia Kawawa, nyumba namba 10.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “JELA MWAKA MMOJA KUMDHALILISHA MAMA YAKE MZAZI”
Post a Comment