Tuesday, November 1, 2016
CHADEMA YAUKATAA MUSWAADA WA VYOMBO VYA HABARI
Do you like this story?
Chama cha Demokrasia na Maendeleo,
CHADEMA kimesema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari
unaotarajiwa kuwasilishwa kwenye Mkutano wa Bunge unaoanza leo Jumanne, Novemba
1, mwaka huu, ni hatari.
Chama hicho katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari, kimesema kuwa serikali inapaswa kutoa muda zaidi kwa wadau
kuujadili ili kushauri na kuondoa mambo ambayo ni hatarishi katika tasnia ya
habari nchini.
"Kutokana na Serikali kuamua
kupuuza maoni ya wadau na wananchi kwa ujumla kuhusu kuongeza muda wa kujadili
na kuboresha Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari, ambao iwapo utaachwa na
kupitishwa kama ulivyo unalenga kutunga sheria hatari zaidi dhidi ya vyombo vya
habari, haki ya wananchi ya kupata taarifa na hata uhuru wa kutoa maoni"
Kamati Kuu ya Chama hicho katika kikao
chake cha kawaida kilichoketi Oktoba 22-23, Jijini Dar es Salaam, pamoja na
masuala mengine, imetuma ujumbe wa baadhi ya wajumbe waandamizi wa Kamati
hiyo kwenda mjini Dodoma kukutana na Wabunge wa CHADEMA, ili kujadiliana
na kutoa maelekezo ya Chama kuhusu muswada huo.
Tundu Lissu
Katika hatua nyingine, chama hicho
kimetangaza majina ya wabunge waliochaguliwa kuingia katika Kamati Kuu ya chama
hicho kupitia tiketi ya ubunge wao, katika uchaguzi uliofanyika Jumapili,
Oktoba 30, mwaka huu, mjini Dodoma.
Wajumbe waliochaguliwa ni pamoja na
1. Tundu Antipas Lissu
2. Godblesss Jonathan Lema
3. Joseph Osmund Mbilinyi
4. Ester Amos Bulaya
5. Mariam Salum Msabaha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “CHADEMA YAUKATAA MUSWAADA WA VYOMBO VYA HABARI”
Post a Comment