Tuesday, November 1, 2016
MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KUANZA LEO... NECTA YATOA ONYO KALI
Do you like this story?
Watahiniwa
408,442 wamesajiliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) kufanya Mtihani wa
Kidato cha Nne unaotarajia kuanza leo hadi Novemba 18, mwaka huu.
Akizungumzia
maandalizi ya mtihani huo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema
kati ya watahiniwa waliosajiliwa wa shule ni 355,995 na wa kujitegemea ni
52,447. Mwaka 2015, waliosajiliwa kufanya mtihani ni 448,382, hivyo kuwapo na
upungufu wa watahiniwa 39,940.
Dk
Msonde alisema kati ya watahiniwa wa shule 355,447 waliosajiliwa, wavulana ni
173,423 ambao ni asilimia 48.72 na wasichana ni 182,572 sawa na asilimia 51.28.
Watahiniwa 59 ni wasioona na wenye uoni hafifu ni 283.
Alisema
kati ya watahiniwa wa kujitegemea 52,447 waliosajiliwa, wanaume ni 25,529 sawa
na asilimia 48.68 na wanawake ni 26,918 sawa na asilimia 51.32.
Pia
watahiniwa wa kujitegemea wasioona wako saba, wanawake watatu na wanaume ni
wanne. Mwaka jana watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 54,317.
Kuhusu
watahiniwa waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Maarifa (QT), Dk Msonde alisema
baraza limesajili 20,634 ambao wanaume ni 7,819 sawa na asilimia 37.89 na
wanawake ni 12,815 sawa na asilimia 62.11. Mwaka jana, idadi ya watahiniwa wa
QT walikuwa 19,547.
“Maandalizi
yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na usambazaji wa
mtihani, vitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo
katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani,” alieleza Dk Msonde.
Aidha,
baraza limewaasa wanafunzi, walimu kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu wa
mtihani kwani watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali
zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufutiwa matokeo yote.
Katika
matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa wiki iliyopita, wanafunzi 238 kutoka
shule sita walifutiwa matokeo yao yote kutokana na udanganyifu wa mtihani.
Dk
Msonde alizitaka Kamati za Mitihani za Mikoa na Halmashauri, kuhakikisha kuwa
taratibu zote za uendeshaji mitihani ya Taifa zinazingatiwa ipasavyo, ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha kuwa mazingira ya vituo yapo salama, tulivu na kuzuia
mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu. Pia Dk Msonde alitoa mwito kwa
wasimamizi wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.
“Wasimamizi
wanaaswa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani baraza litachukua hatua
kali kwa yeyote yule atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa Mitihani
ya Taifa,” alieleza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KUANZA LEO... NECTA YATOA ONYO KALI”
Post a Comment