Sunday, November 6, 2016
SIMBA WAANGAMIZWA NA AFRICAN LYON
Do you like this story?
Simba
SC waliingia mchezoni wakijiamini vyema dhidi ya African Lyon kwa mwendelezo
mzuri wa matokeo ya nyuma.
Hesabu
za Bernardo mreno wa African Lyon zilitofautiana na Joseph Omog kocha mkuu wa
Simba SC . Bernado alijipanga kuzuia na kushambulia kwa kuvizia lakini mahesabu
makubwa katika kuzuia aliwapanga vijana wake kukabia juu ya mstari na sio
kupaki basi katika mfumo wao wa 4-4-1-1 waliokuwa wakiutumia lakini pia
wakichanganya na 4-5-1 ili kuvunja maelewano ya viungo wa Simba SC pale kati.
Omog
kwa asilimia nyingi alijipanga kushambulia pande zote. Alimweka Mwinyi Kazimoto
kushoto kama kiungo mchezeshaji wa pembeni pia kiungo mshambuliaji kificho
akitumia 4-4-2. Kichuya kulia na Mzamiru Yassin kama mchezeshaji nyuma ya
Mohamedi Ibrahimu . Wote hawa ni wana uwezo mzuri wa kukaa na mpira na
kushambulia lakini ubora wao unategemea kiungo cha chini kimejipanga vipi pia
wing backs wanasaidia vipi mashambulizi hayo.
African
Lyon walichofanya ni kuhakikisha Jonasi Mkude anakosa mawasiliano mazuri na
Mzamiru Yassini ili kuvunja mawasiliano ya kati kwa kiungo na safu ya
ushambuliaji .
Walipokuwa
wakipoteza mpira Lyon wananadilika kutoka 4-4-1-1 na kucheza 4-5-1 ili Kuziba
njia za mpira na kupunguza eneo la kucheza kwa Simba SC kujipanga kwa
mashambulizi.
Lyon
walidhamiria kuwakataa Simba SC kwenye kwenye pasi fupi fupi za haraka kuja
langoni mwao ( direct play ) na kuwalazimisha wacheze sana kwenye eneo lao kwa
squre passes na wakijaribu kusogea juu watumie mipira mirefu ambayo mara nyingi
si mizuri kujenga mashambulizi.
Mbinu
hizi zilimfanya mshambuliaji wa Simba SC Laudit Mavugo kushindwa kupata mipira
na muda mwingi kuwa off target mpaka alipotolewa na kuingia Saidi Ndemla.
Mashambulizi
ya kuvizia yaliwapa goli la jioni Lyon wakifanikiwa kwenye mbinu zao .
Walilenga kujilinda na kushambulia kwa kushitukiza lakini mfumo wao wa
kujilinda ndio uliowafanya Simba SC kupotea uwanjani kwa kukabia juu.
Samuel
Samuel
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)



0 Responses to “SIMBA WAANGAMIZWA NA AFRICAN LYON”
Post a Comment