Sunday, November 6, 2016
YANGA WAONDOKA NA POINTI TATU MUHIMU MBEYA
Do you like this story?
Yanga
SC leo wamejitutumua na kufuta makosa yao dhidi ya Prison ya Mbeya na
kufanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa bao pakee la penati katika mchezo
uliofanyika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Katika
mchezo huo ambao ulikuwa mkali na wa kusisimua, kila timu ilianza kucheza kwa
tahadhari kubwa ili kutoruhusu bao la mapema na kujiweka katika mazingira
magumu.
Dakika
ya 32, Mbuyu Twite alilimwa kadi ya njano baada ya kumfanyia faulo Benjamin
Asukile na mwamuzi kumpa adhabu hiyo.
Dakika
ya 45 kinda wa Yanga Yusufu Mhilu alikosa bao baada ya shuti lake kupaa nje ya
lango la Prisons.
Kipindi
cha kwanza kiliisha huku kila upande ukitoka bila kuona lango la mpinzani wake.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi kutokana na Prisons kuamua kushambulia hali
iliyopelekea mchezo kuwa mgumu kwa pande zote mbili.
Kutokana
na hali kuzidi kuwa ngumu Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Yusufu Mhilu na
nafasi yake kuchukuliwa na Simon Msuva.
Prisons
walipata penati baada ya Deus Kaseke kufanya madhambi katika eneo la hatari,
lakini penati iliyopigwa na Lambert Sabianka iliokolewa na Beno Kakolanya.
Dakika
ya 60 Amissi Tambwe aliingia kuchukua nafasi ya Deus Kaseke.
Yanga
walipata penati kufuatia mshambuliaji wao Mzambia Obrey Chirwa kuangushwa
kwenye eneo la penati na Simon Msuva kuukwamisha mpira wavuni na kuipa Yanga
bao la ushindi.
Mwamuzi
alikataa kutoa penati kwa Yanga baada ya Donald Ngoma kufanyiwa faulo ya wazi
na beki wa Prison dakika za majeruhi.
Mpaka
filimbi ya mwisho inapulizwa, Yanga waliibuka kifua mbele kwa ushindi wa bao
1-0. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kuwa mbabe wa Prisons baada ya
kuibuka na ushindi katika michezo mingi waliyokutana hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “YANGA WAONDOKA NA POINTI TATU MUHIMU MBEYA”
Post a Comment