Friday, February 24, 2017

NGULI WA KISWAHILI AFARIKI



Msomi maarufu wa lugha ya kiswahili Sheikh Ahmed Nabhany amefariki akiwa na umri wa miaka 90.
Marehemu alifariki mapema siku ya Alhamisi na anatarajiwa kuzikwa mwendo wa saa kumi na moja jioni katika makaburi ya Matondoni mjini Lamu.
Viongozi kadhaa wakuu ikiwemo wasomi wa Kiswahili pamoja na wapenzi wa lugha hiyo nchini Kenya wanatarajiwa kuhudhuria mazishi yake.
Sheikh Nabhany ambaye anatambuliwa kama Profesa na wengi, ikiwemo wanafunzi wake duniani alihamia nyumbani kwake Matondoni kutoka mji wa kale Mombasa kutokana na uzee na kuugua.
Akiwa mshindi wa tuzo ya rais ya Golden Warrior ODW, Sheikh Nabhany alizaliwa mjini Amu{ Lamu} mwaka 1927 na kujifunza katika madrassa.
Nabhany anayetambuliwa kuwa mshairi wa kiswahili na msomi, alianza masomo yake mjini Lamu na kujifunza ushairi kutoka kwa bibiye.
Amewasaidia wasomi wengi katika utafiti wao na kufanya kazi kupitia tamaduni kadhaa za kiswahili.
Msomi huyo alichangia maendeleo ya kiswahili na amekuwa akitembelea vyuo vikuu vya Marekani na Ujerumani miongoni mwa mataifa mengine.
Alikua mtetezi mkubwa wa kiswahili na mara nyingi alitembelea na hata kupiga simu katika vyombo kadhaa vya habari mbali na waandishi ili kutoa ushauri wake kuhusu utumizi wa maneno yanayohitajika hususan katika teknolojia.
Alikuwa mwalimu wa wanafunzi wengi katika vyuo kadhaa vya Ulaya ambao walitembelea makaazi yake katika eneo la mji wa kale mjini Mombasa katika tafiti zao.

0 Responses to “NGULI WA KISWAHILI AFARIKI”

Post a Comment

More to Read