Wednesday, April 5, 2017

HATUA KUMI ZA KUFUATA (Pamoja na Picha) UNAPOFUNGUA CHUPA YA SHAMPENI (Champagne)



 1.Kabla ya kuanza kufungua, hakikisha  chupa yenye shampeni imehifadhiwa kwenye ubaridi kwa muda Fulani kwani kinywaji hiki ni bora zaidi kikinywewa kikiwa baridi. Unaweza usiweke kwenye baridi kama tu unataka shampeni iruke sana na kusambaa kila mahali. 





  2.Itoe Shampeni kwenye Jokofu au mahali popote ulipoihifadhi, Futa chupa na kitambaa lain (kisafi) Kuzuia Kuteleza mikononi mwako.






 
 
 
 
 3. Ondoa Karatati inayozunguka shingo na mdomo wa chupa ya shampeni. Ili kuondoa Karatasi hiyo, zungusha chupa yako na kutazama kiungio cha karatasi hiyo na kuivuta taratibu. 

  


  4.Utaona waya uliosukwa kuzunguka  kizibo cha chupa ya shampeni. Waya huo unazuia kizibo  hicho kisitoke kunapokuwa na presha kubwa, joto, au mtikisiko.   

  5.Weka kidole gumba  cha mkono uliotumia kushika shingo  ya chupa ya shampeni, tumia mkono wako mwingine kuondoa  waya  unaozunguka kifuniko cha chupa.
 Kumbuka waya huo huondolewa kwa kuzungusha ukianzia sehemu ya pembeni iliyofungwa kama kitanzi.


 
  6.Ondoa waya na kuuweka pembeni. Bila kuachia kizibo, Unaweza Kutikisa chupa  mara kadhaa kama unataka shampeni iruke. Kama hutaki iruke basi usitikise chupa hiyo. 





  
 
7. Weka kitako cha chupa Tumboni kwako ili kuipa balance huku mdomo wa chupa ukiangalia juu kwa nyuzi 45 (45 degrees). Hii itazuia kizibo au shampeni kumrukia mtu aliyeko karibu wala wewe.


8.Achia Kidole kilicho juu ya kizibo, Huku mkono wako mmoja ukiwa umeshika shingo ya chupa (usiielekeze chupa kwa mtu) na mwingine ukiwa huru. 



   
 
 
 
 
9. Anza kuzungusha kizibo cha chupa taratibu kulia na kushoto huku ukikivuta taratibu sana mpaka kitoke. Kumbuka unaweza kukiachia kiruke au kukishikilia kama ni tafrija inayohitaji utulivu sana. 





 10.Hongera, umeshajua Kufungua Shampeni. Nyanyua chupa  juu, na kuanza kugawa kwa watu. 

0 Responses to “HATUA KUMI ZA KUFUATA (Pamoja na Picha) UNAPOFUNGUA CHUPA YA SHAMPENI (Champagne) ”

Post a Comment

More to Read