Wednesday, April 5, 2017
SHERIA 10 ZA AJABU ZA BARABARANI UKITEMBELEA NCHI HIZI
Do you like this story?
Najua nina watu wangu ambao ni watembezi katika miji mbalimbali
duniani na watataka kufahamu sheria za barabarani zinazotumika katika
miji hiyo.
Sasa hapa nimekusogezea sheria 10 ambazo hutakiwi kuzivunja uendeshapo gari katika miji hii.
1: Chenzhen, China
Katika mji wa Chenzhen uliopo China dereva wa gari akikamatwa na kosa la kuwasha taa ‘full light’
bila sababu ya msingi adhabu yake ni kukaa mbele ya gari lililowashwa
taa kwa dakika moja na kulipa fine ya Dollar 30. Adhabu hii imewekwa
kama funzo kwa madereva ili kujua athari za kumuwashia mtu mwingine taa
bila sababu.
2: Manila, Ufilipino
Katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila madereva wote wenye gari zenye
plate number zinazoishia na namba mbili au moja hawaruhusiwi kuendesha
gari siku za Jumatatu.
3: Arkansas, Marekani
Katika mji wa Arkansas uliopo Marekani ni kosa kisheria dereva kupiga
honi akiwa maeneo yanayouzwa vinywaji baridi au katika vibanda vya
kuuza sandwiches baada ya saa tatu usiku.
4: Colorado, Marekani
Ni marufuku kuendesha gari lenye rangi nyeusi siku za Jumapili ukiwa katika mji wa Colorado.
5: New Orlens, Marekani
Katika mji wa New Orlens, Marekani mwanamke harusiwi kuendesha gari
mpaka mwanaume asimame mbele ya gari akiwa na bendera nyekundu ili kutoa
angalizo kuwa kuna mwanamke anataka kuendesha gari hilo.
6: Ujerumani
Ni kosa la kisheria kuishiwa mafuta ukiwa unaendesha gari Ujerumani.
Sheria hii imewekwa ili kuondoa magari ambayo yanasimamishwa barabarani
kwa kisingizio cha kuishiwa mafuta.
7: Sweden
Nchini Sweden ni marafuku kuzima taa za gari hata ikiwa mchana.
Madereva wa nchi hiyo wanatakiwa kuwasha taa za gari saa 24 hata ikiwa
mwezi June ambapo jua huwa halizami katika maeneo mengi nchi humo.
8: California, Marekani
Ukiwa katika mji wa California ni kosa kwa wanawake kuendesha gari
wakiwa wamevaa nguo za kulalia. Sheria hii ilikuja baada ya wanawake
wengi kuvaa pajama hasa nyakati za asubuhi wakiwa wanapeleka watoto
shule. Mtu atakayekiuka sheria hii anapigwa fine ya Dollar 22.
9: New Britain, Marekani
Ni kosa kuendesha gari kwa kasi 25 mhn hata ikiwa ni gari la zimamoto linawahi kuzima moto sehemu yoyote.
10: North Carolina, Marekani
Katika mji wa North Carolina, Marekani ni kosa kwa dereva kuendesha gari pembezoni mwa makaburi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SHERIA 10 ZA AJABU ZA BARABARANI UKITEMBELEA NCHI HIZI”
Post a Comment