Wednesday, April 5, 2017
SERIKALI KUTATAUA KERO YA MAJI CHALINZE
Do you like this story?
Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa
China, Benki ya Maendeleo ya Waarabu(BADEA),Washirika wa Maendeleo
(DPS), na Serikali ya India kwa pamoja wametoa jumla ya Shillingi
Billion 164 kawa ajili ya kutekeleza mradi wa maji Chalinze kwa awamu
tatu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson
Lwenge wakati akijibu Swali Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete
alilouliza kuwa Wakazi wa Chalinze wamekuwa katika sintofahamu ya
kukamilka kwa mradi wa maji Chalinze.
Amesema kuwa Serikali ipo katika utekelezaji wa mradi huo na gharama
za utekelzaji wake ni Shillingi Billioni 23.4 kwa awamu ya kwanza na
Shillingi Billioni 53.7 kwa awamu ya pili ya mradi na kwa awamu ya tatu
itagharimu Shillingi Billioni 86.9.
Aidha, ameongeza kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza na utekelezaji
umekamilika na kwa awamu ya pili ya mradi huo jumla ya vijiji 88
vimenufaika na kupeleka hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa
Chalinze na Vitongoji vyake kufikia asilimi 88 ya wakazi wote waishio
katika eneo lote linalopitiwa na mtandao wa maji.
“Mradi upo katika hatua nzuri na umekamilika kwa awamu ya kwanza na
awamu ya pili ipo katika utekelzeaji na wanachi wameanza kunufaika na
mradi huu kwa kupata huduma ya maji” amesema Lwenge.
Pia amesema kuwa katika awamu ya pili vijiji 12 vya Mwindu,Visakazi,
Lulenge, tukamisasa,Kinonko, Bwawani, Sinyaulime, Gwata, Ngerengere,
Kidugalo, Kambi ya Kinonko na Sangasanga vitaanza kupata huduma ya maji
ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka 2017 baada ya kukamilika kwa
majaribio ya bomba kuu.
Vijiji vitatu vya Kwang’andu,kifuleta na Kwaruhombo vitaanza kupata
maji mara baada ya mkandarasi kufanya maboresho ya pampu ambazo
zimeonekana hazifanyi kazi kama inavyotakiwa na mkandarasi huyo
ameagizwa kuhakikisha pampu hizo zinafanya kazi kabla ya Juni 2017.
Hata hivyo, ameongeza kuwa kwa sasa Serikali inatekeleza mradi huo
kwa awamu ya tatu ambapo upanuzi wa mtambo wa kuzalisha maji, ujenzi wa
mabomba makuu ya kusafirisha maji (KM 115), Ujenzi wa mfumo wa manomba
ya kusambaza maji(KM 1022), Ujenzi wa matanki makubwa 19 na ujenzi wa
vituo 9 vya kuchotea maji na ujenzi wa vioski 351 vya kuchotea maji
vinatekelzwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI KUTATAUA KERO YA MAJI CHALINZE”
Post a Comment