Wednesday, April 5, 2017
KITILA,SEMAKAFU WALA KIAPO MBELE YA JPM
Do you like this story?
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha viongozi
aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali.
Rais John Pombe Magufuli akimwapisha Prof. Kitilia Alexander Mkumbo kuwa katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es salaam April 5,2017
Hafla ya kuapishwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Dkt. Magufuli amemuapishwa Dkt. Leonard Douglas Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Prof. Kitila Alexander Mkumbo ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Dkt. Ave Maria Emilius Semakafu ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Mhe. Baraka Haran Luvanda ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini India.
Mhe. Sylvester Mwakinyuke Ambokile ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akimwapisha Dkt. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam April 5,2017
Bw. Charles Edward Kichere ameapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Aidha, Viongozi hao wamekula kiapo cha
uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Katibu wa Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Waziri Yahaya Kipacha.
Akizungumza baada ya kuapishwa kwa
viongozi hao, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapongeza kwa
kuteuliwa kushika nyadhifa hizo na amewataka kufanya kazi kwa
kutanguliza maslai ya Taifa na kwa kuzingatia sheria na taratibu
zilizowekwa.
“Tutawapa ushirikiano wote
mtakaouhitaji ili kufanikisha kazi zenu lakini na nyinyi msituangushe,
Bw. Kichere tunakutegemea ukaimarishe ukusanyaji wa mapato pale TRA na
pia ukawaambie maafisa wako na mameneja wa mikoa waache kutoa kauli za
kuigombanisha Serikali na wafanyabiashara, wakusanye kodi kwa kufuata
sheria na taratibu na pia wawe na lugha nzuri.
“Prof. Kitila Mkumbo tunategemea utaongeza msukumo kutatua matatizo ya maji, utasaidia kufanikisha kampeni ya kumtua Mama ndoo ya maji, Watanzania wapate maji safi na salama” amesema Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
“Prof. Kitila Mkumbo tunategemea utaongeza msukumo kutatua matatizo ya maji, utasaidia kufanikisha kampeni ya kumtua Mama ndoo ya maji, Watanzania wapate maji safi na salama” amesema Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muunganoi wa Tanzani Mhe. Samia Hassan Suluhu, Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Kamshna wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania TRA Charles Edward Kichele, Balozi wa Tanzania nchini
Idia Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Sylvester
Ambokile Mwakinyuke, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na
Teknolojia Ave Maria Semakafu, Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na
Umwagiliaji Prof. Kitilia Alexander Mkumbo na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia mara baada ya kuapishwa na Rais Ikulu
Jijini Dar es salaam April 5,2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KITILA,SEMAKAFU WALA KIAPO MBELE YA JPM”
Post a Comment