Wednesday, April 5, 2017
TAKRIBANI WATU 9 WAHOFIWA KUFA MAJI ZANZIBAR
Do you like this story?
Watu 9 hawajulikani waliko huku 44 waliokolewa baada ya mashua yao ya uvuvi kuzama nje ya pwani ya kisiwa cha Zanzibar.
Makarani
Mohamed, ambaye ni kaimu mkurugenzi ya kitengo cha ujajususi aliambi
BBC kuwa shughuli ya kutafuta na kuwaokoa watu bado inaendelea."Tunafahamu, kuwa ajali hiyo ilisababishwa na upepo na mawimbi makali yaliyosababisha mashua hiyo kuzama.Alisema.
Manusura mmoja waliwaambia waokoaji kuwa takriban watu 53 waliondoka kuenda kuvua samaki jana jioni wakati bahari ilikuwa tulivu.
Lakiki hali ya hewa ilibadilika na kusababisha mawimbi makali ya bahari.
Alisema kuwa hajawaona wenzake tangu ajali hiyo itokee.
Uvuvi ni shughuli kubwa ya kiuchumi katika kisiwa cha Zanzibar lakina mashua nyingi huwa zimechakaa hali ambayo husababisha ajali nyingi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAKRIBANI WATU 9 WAHOFIWA KUFA MAJI ZANZIBAR”
Post a Comment