Thursday, April 3, 2014

BODABODA WAANDAMANA MTWARA.





Madereva pikipiki maarufu kama bodaboda mkoani hapa, wameandamana hadi Kituo Kikuu cha Polisi wakipinga hatua ya polisi kuwakamata na kuwapiga.
Maandamano hayo yalisababisha shughuli mbalimbali kusimama baada ya polisi kuingilia kati na kuyatuliza kwa vile hayakupata kibali.

Hofu miongoni mwa wananchi ilikuwa kubwa kutokana na polisi kutanda sehemu mbalimbali.
Mashuhuda walisema kuwa polisi walalizimika kuingilia kati ili kuwatawanya madereva hao wa bodaboda na kuleta hofu kubwa.
Madereva hao wanadai kuwa askari wa usalama barabarani wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuwakamata na kuwapiga bila sababu za msingi. Mmoja kati ya madereva hao ambaye hakutaka jina lake kuandikwa kwenye gazeti, alisema walikaa kikao na polisi na kuafikiana kila dereva kuwa na kofia ya kuvaa kichwani pamoja na abiria atakayembeba.

“Tulikubaliana baada ya miezi mitatu kila dereva lazima awe na kofia ya usalama kuvaa kichwani,” alisema.
“Tumeshangazwa na hatua ya polisi kuanza kutukamata kabla hata ya muda tuliokubaliana kufika.”

0 Responses to “BODABODA WAANDAMANA MTWARA.”

Post a Comment

More to Read