Thursday, April 3, 2014
SERIKALI YATANGAZA KUWAGAWIA WANAFUNZI KONDOMU ILI WAFANYE NGONO KWA RAHA.
Do you like this story?
Serikali
ya Afrika Kusini imeanza mpango wa kuwapa vijana wa shule za sekondari
kuendelea juu mipira ya Condom zenye rangi tofauti tofauti na ambazo zina
harufu nzuri ya kuvutia.
Mpango
huu unalenga kuzuia wanafunzi kuchoka kutumia mipira ya kawaida ya condom
wanaposhiriki ngono.
Waziri
wa afya Aaron Motsoaledi, ameyasema hayo baada ya utafiti uliofanywa nchini
humo kuonyesha kuwa matumizi ya mipira ya Condom imepungua nchini Afrika
Kusini.
Inaarifiwa
kinachosababisha upungufu huo ni kwamba Condom za kawaida zinazotolewa na
serikali hazina mvuto wowote kwa vijana.
Afrika
Kusini ina watu milioni 6.4 wanaoishi na virusi vya HIV, idadi hiyo ikiwa juu
zaidi kuliko nchi yoyote duniani.
Utafiti
uliofanywa na kitengo cha serikali cha utafiti wa afya, ulionyesha maambukizi
yameongezeka hadi asilimia 12.2.
Takriban
watu milioni 2 hupata matibabu ya ARV's au madawa ya kupunguza makali ya HIV.
Hata
hivyo baadhi ya mashirika ya misadaa yanaonya kuwa baadhi ya kliniki
zinakabiliwa na upungufu wa dawa hizo.
Condom
hizo zitatolewa na serikali kwa vijana bila malipo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YATANGAZA KUWAGAWIA WANAFUNZI KONDOMU ILI WAFANYE NGONO KWA RAHA.”
Post a Comment