Monday, January 11, 2016
FIFA YAITAKA ETOILE KUILIPA SIMBA HARAKA
Do you like this story?
Kamati
ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) iliyokutana Disemba
15 mwaka jana, imeiagiza klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kuilipa Simba SC
ya Tanzania pesa za uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi ndani ya siku sitini
(60) kuanzia Januari 7, 2016.
Katika
taarifa hiyo ya FIFA na nakala yake kutumwa kwa TFF, Etoile du Sahel na Simba
SC, Kamati ya Nidhamu imefikia uamuzi huo baada ya klabu ya Etoile du Sahel
kupuuza kuilipa klabu ya Simba SC kiasi cha dola za kimarekani 300,000 za
uhamisho wa mchezaji wa Emmanuel Okwi uliofayika Januari 2014.
Katika
barua hiyo ya maamuzi ya kikao hicho, Kamati ya Nidhamu imesema baada ya siku
sitini (60) zilizotolewa kwa klabu ya Etoile kuwa imeilipa Simba SC kumalizika
bila malipo hayo kuwa yamaefanyika, wataagiza Etoile du Sahel kukatwa pointi
sita katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Tunisia.
Na
kama klabu ya Etoile itashindwa kulipa deni hilo hata baada ya kukatwa pointi
sita, Kamati ya Nidhamu ya FIFA itaamua kuishusha daraja klabu hiyo kutoka Ligi
Kuu mpaka ligi daraja la kwanza.
Chama
cha Soka nchini Tunisia (FTF) kimekumbushwa kutekeleza maelekezo hayo ya Kamati
ya Nidhamu ya FIFA ya kuipokonya pointi sita Etoile du Sahel, na endapo FTF
itashindwa kufanya hivyo basi itafungiwa kujishugulisha na shughuli zote za
mpira zinazosimamiwa na FIFA.
Aidha
Kamati ya Nidhamu ya FIFA pia imeigiza klabu ya Etoile du Sahel kulipa faini ya
dola za kimarekani 20,000 ndani ya siku sitini (60) baada ya kupokea uamuzi huo
wa kamati.
TFF
imepewa jukumu la kuhakikisha Simba inalipwa deni hilo ndani ya muda uliopangwa
wa siku sitini (60) na endapo klabu ya Etoile du Sahel itashindawa kufanya
hivyo basi TFF iitarifu kamati ya nidhamu ya FIFA juu ya suala hilo.
Kikao
hicho cha Kamati ya Nidhamu kiliiongozwa na Mwenyekiti Claudio Sulser (Uswisi),
Makamu Mwenyekiti Kia Tong Lim (Singapore), na mjumbe Fiti Sunia (Visiwa vya
Samoa)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “FIFA YAITAKA ETOILE KUILIPA SIMBA HARAKA ”
Post a Comment