Monday, January 11, 2016

JK AMPONGEZA SAMATTA KWA TUZO YA AFRKA


Kikwete na Samatta wakiongozana kutoka ndani ya Ofisi za CCM, Lumumba jijini Dar.

Waziri Nape Nnauye akizungumza jambo.

Akiagana na Viongozi hao.

Akipanda kwenye gari tayari kwa kuondoka Lumumba.


RAIS wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, leo amekutana na mwanasoka Mbwana Samatta ambaye anaendelea kupokea pongezi za Watanzania kwa ushujaa wa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa wale wanaocheza soka ndani ya Afrika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Rais  huyo mstaafu amempongeza kwa mafanikio hayo lakini akatoboa siri kuwa yote ni matokeo ya wosia aliompa walipokutana jijini Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo alimtaka awaze mafanikio ya juu zaidi hasa kucheza Ulaya badala ya kujiona kama amefika akiwa na kikosi cha TP Mazembe.

Katika mkutano na waadishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mtaa wa  Lumumba jijini Dar es Salaam, Kikwete alisema ana kila sababu ya kumpongeza mshambuliaji huyo ambaye anaelekea kwenda kucheza soka katika klabu ya Genk ya Ubelgiji kwani ndiye mkombozi wa taifa ambalo limekuwa na ukame kwenye michezo huku akiiomba wizara  husika ya michezo kuhakikisha wanamsaidia katika kila hatua.

“Tanzania tumekosa furaha muda mrefu kwenye michezo, tumekosa makombe miaka mingi, lakini Samatta leo hii ametuinua kwa kuleta tuzo hii. Lazima tumpongeze.

“Nilikutana naye Kinshasa ambako nilimisihi sana alenge juu zaidi na sio Mazembe tu na shabaha kubwa iwe ni Ulaya ili nasi siku moja tumuone kwenye runinga akicheka na nyavu.

 Alitekeleza nilichomwambia na kweli timu nyingi leo hii zinamtaka huko Ulaya. Nimeomba wizara ya michezo waone jinsi ya kumsaidia katika kila hatua atakayopiga,” alisema kiongozi huyo wa zamani.

Kwa upande wa Samatta amempongeza Kikwete na serikali yake ya  awamu ya nne kwa kuwa naye bega kwa bega kwa kila hatua aliyoipiga.

Aidha Samatta alimkabidhi JK zawadi ya jezi ya TP Mazembe Na. 9 aliyokuwa akivaa klabuni hapo ambayo anaiacha baada ya kupata dili Ubelgiji anakoelekea sasa.
PICHA NA MUSA MATEJA/GPL

0 Responses to “ JK AMPONGEZA SAMATTA KWA TUZO YA AFRKA”

Post a Comment

More to Read