Monday, January 11, 2016

KIJANA WA MIAKA 26 AUA MKEWE WA MIAKA 40 KWA WIVU WA MAPENZI


  Kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa Bw Peter Kakamba


JESHI  la  polisi  mkoa  wa Iringa linamshikilia Bw James Benitho (26) mkazi mmoja  wa  kijiji  cha Iyegela   wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa kwa  tuhuma  za  kumuua mkewake mwenye umri  wa miaka 40  kwa kumnyonga na kumchoma na kitu  chenye ncha kali katika paja  lake  kisha kumzika katika shimo la choo kwa  kile  kinachoelezwa na wivu  wa kimapenzi.

Imeelezwa    kuwa mwanaume   huyo Bw Benitho  alifikia uamuzi   huwa  wa kufanya mauwaji  hayo ya  kinyama  dhidi ya  mkewe  baada ya kubaini kusalitiwa ndoa yake  kwa mwanamke   huyo kuwa na mahusiano ya  kimapenzi na mwanaume  mwingine.

Kamanda  wa  polisi wa  mkoa  wa Iringa  Peter  Kakamba  ameeleza kuwa leo   kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa moja asubuhi baada ya mwili    wa mwanamke  huyo kukutwa katika  shimo la choo cha mtuhumiwa  huyo.

Kamanda Kakamba  alisema  kuwa  baada ya  mtuhumiwa   huyo kukamatwa alikili  kutenda kosa   hilo la mauwaji na  kuwa alifanya mauwaji hayo January 2 mwaka huu majira  ya  usiku huku akidai kuwa alifanya   hivyo kutokana na wivu  wa mapenzi .

Hata   hivyo  alimtaja  mwanamke  huyo  aliyeuwawa kuwa ni Lucy Mhusi (40) ambae ni mkulima  wa  kijiji  hicho aliyekutwa katika shimo  la choo juzi akiwa ameuwawa kwa  kuchomwa na  kitu  chenye ncha kali katika paja  la  mguu  wake  wa  kushoto  na  kunyongwa  shingo kabla ya kuzikwa katika shimo  la  choo na kuwa mtuhumiwa  huyo  amekamatwa na atafikishwa mahakamani  wakati  wowote  kuanzia sasa kwa tuhuma  za mauwaji hayo .

Wakati  huo  huo mtoto Heren Mhenzi (5) mkazi  wa Isele  kata ya llula  barabara  ya Ilula Image   wilaya ya Kilolo  amepoteza maisha  yake baada ya  kugongwa na  pikipiki yenye namba  za usajili  MC156 ASR ikiendeshwa na  Goshen Lutambi (25) mkulima   mkazi wa Mtuwa ilimgonga  mtoto   huyo na  kusababusha kifo chake papo  hapo na  kuwa  chanzo ni mwendo kasi na  dereva  kutochukua  tahadhali za barabarani .

Kamanda Kakamba alisema  kuwa jeshi  la  polisi halitaacha  kuchukua hatua kali  dhidi ya madereva  boda boda  ambao baadhi yao wamekuwa  wakiendesha  vyombo   hivyo  pasipo  kuzingatia sheria  za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuendesha kwa  mwendo kasi jambo ambalo ni hatari kwao na watumiaji  wengine wa barabara.

0 Responses to “KIJANA WA MIAKA 26 AUA MKEWE WA MIAKA 40 KWA WIVU WA MAPENZI”

Post a Comment

More to Read