Saturday, December 31, 2016
IDADI NA AINA YA WAHALIFU WA MTANDAO WALIOKAMATWA KUPITIAKITENGO MAALUMU CHA UCHUNGUZI WA MAKOSA YA JINAI YA KIMTANDAO
Do you like this story?
Serikali kupitia kitengo maalum cha uchunguzi wa jinai ya
kimtandao, imefanikiwa kukamata watuhumiwa 690 kwa tuhuma za kufanya uhalifu wa
mtandao.
Watuhumiwa hao ni matapeli, wezi, waporaji wa simu za mkononi na wengineo
wanaotumia mfumo wa intaneti kuibia watu wasiokuwa na hatia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projestus
Rwegasira alisema juzi jioni kuwa ofisi yake imekuwa ikikabiliana kikamilifu na
wahalifu hao.
Alisitiza kwamba wahusika wote wa vitendo hivyo, watakamatwa. Meja
Jenerali Rwegasira alikuwa akizungumza katika mahojiano katika kipindi cha
Tunatekeleza, kinachorushwa na Televisheni ya Taifa(TBC). Kwamba wizara yake
kwa kushirikiana na vyombo vya serikali, inaandaa mashtaka dhidi ya watuhumiwa
waliokamatwa na watafikishwa mahakamani.
“Tunafanya kila juhudi kuzuia vitendo vya uhalifu wa kimtandao,
tayari tumekamata baadhi ya watuhumiwa na watakabiliana na mkono wa sheria
mahakamani,” alisema.
Alisema serikali imeunda kitengo maalumu chini ya Wizara ya Mambo
ya Ndani, kukabiliana na udanganyifu na uhalifu wa kimtandao nchini na kimekuwa
kikifanya kazi nzuri.
Rwegasira alisema, “Ningependa kuutangazia umma kuwa huru kutoa
taarifa ya vitendo kama hivyo polisi mara wanapoona, tuna uwezo wa kufuatilia
simu zilizoibwa na kuwakamata watuhumiwa”.
Mwezi Januari mwaka huu, Mkuu wa Kitengo cha Sheria katika Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Veronica Sudayi alisema tangu kupitishwa
kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao na Miamala ya Kielektroniki ya 2015 mwezi
Septemba 2015, kiwango cha wizi na udanganyifu nchini, kimepungua kwa asilimia
60.
Sudayi alisema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi
wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuhusu Sheria hiyo ya Makosa ya
Mtandao. Kuhusu amani na usalama, katibu mkuu huyo alisema serikali imejiandaa
vya kutosha kulinda watu na mali zao na kujipanga vya kutosha.
Alisema jeshi la polisi liliweza kukabiliana na changamoto za
kiusalama katika mikoa ya Tanga na Mwanza baada ya watu wasiokuwa na hatia
kuuawa na majambazi. Alisema katika tukio la Tanga, watuhumiwa 28 walikamatwa
na wengine nane walikamatwa kuhusiana na tukio la Mwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “IDADI NA AINA YA WAHALIFU WA MTANDAO WALIOKAMATWA KUPITIAKITENGO MAALUMU CHA UCHUNGUZI WA MAKOSA YA JINAI YA KIMTANDAO”
Post a Comment