Saturday, December 31, 2016
MSAJILI MKUU WA MAHAKAMA TANZANIA AWATAKA MAHAKIMU KUZINGATIA SHERIA
Do you like this story?
Msajili
Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina Revocati amewataka mahakimu nchini
kuzingatia sheria katika utendaji wao wa kazi hasa katika utoaji wa
dhamana.
Kauli
ya Msajili imekuja wakati kukiwa na malalamiko dhidi ya baadhi ya mahakimu
kuwanyima dhamana washtakiwa ilhali mashtaka yao yanaruhusu.
Aidha,
kauli ya msajili huyo mkuu imekuja wakati mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema wakipambana ili mteja wao apate dhamana baada ya kukwaa kisiki
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Mashtaka
ambayo kwa mujibu wa sheria dhamana zake zimezuiwa ni ya mauaji ya kukusudia,
uhaini, utakatishaji wa fedha, wizi wa kutumia silaha, usafirishaji binadamu na
dawa za kulevya.
Hata
hivyo, Mahakama inaweza kuzuia dhamana endapo kutakuwa na pingamizi la
kisheria, na mara nyingi mapingamizi hayo yamekuwa yakiambatana na hati kutoka
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Msajili
huyo alitoa maagizo hayo jana mjini Moshi alipokuwa akizungumza na mahakimu wa
ngazi zote katika mahakama za mjini Moshi baada ya kumaliza ziara ya kikazi
katika mkoa wa Kilimanjaro.
Taarifa
iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Bernard Mpepo
ilisema msajili huyo waliwataka mahakimu watunze maadili yao ili kujenga imani
kwa jamii.
Msajili
mkuu pia alitembelea Gereza Kuu la Karanga mjini Moshi na kufanya ukaguzi wa
kawaida na kisha kuzungumza na wafungwa, mahabusi na wafanyakazi wa
gereza.
Akiwa
katika gereza hilo, msajili mkuu alisema mkakati wa Mahakama ni kuona wateja
wanapata huduma bora na ya haraka na tayari mahakimu wamepewa malengo ya
kumaliza kesi haraka.
Ili
kuboresha huduma, alisema mwaka 2017 wamekubaliana katika mahakama ya mwanzo,
shauri lolote lisikae zaidi ya miezi sita wakati mahakama ya wilaya na mkoa
shauri lisikae zaidi ya miezi 12.
Pia
mahakama imeingia mkataba na Shirika la Posta kusambaza nakala za hukumu kwa
wateja na nakala ya hukumu itakuwa inamfikia mdau ndani ya siku 21.
Chini
ya mkakati huo, nakala ya mwenendo wa shauri utamfikia mteja wa mahakama ndani
ya siku 21.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MSAJILI MKUU WA MAHAKAMA TANZANIA AWATAKA MAHAKIMU KUZINGATIA SHERIA”
Post a Comment