Wednesday, December 28, 2016

IDADI YA WATANZANIA WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI




Ripoti iliyotolewa na shirika la kuhudumia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI nchini Tanzania, TACAIDS inaeleza kuwa hadi kufikia mwaka 2015 takribani watanzania milioni 1.4 walikuwa wakiishi na virusi vya ukimwi. Idadi hii imeelezwa kuwa ni sawa na asilimia saba (7%) ya watu wote wamaoishi na virusi vya UKIMWI, Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Kati ya watu hao milioni 1.4 wanaoishi na virusi hivyo, inakadiriwa kuwa watu laki nane (800,000) walikuwa wakitumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI (ARVs) hadi kufikia nusu ya kwanza ya mwaka 2016. Hii ni sawa na asilimia 53 ya watu wote wanaoishi na virusi hivyo.

Kuhusu kasi ya maambukizi ya virusi hivyo, takwimu kutoka UNAIDS zinaonyesha kuwa kuwa katika kipindi cha mwaka 2015, takribani watu elfu 54 walipata na maamukizi mapya.

Kufuatia hali hiyo, jitihada mbalimbali ambazo zimefanywa zinaonyesha kuzaa matunda katika kupunguza kasi ya maambukizi mapya ambapo kati ya mwaka 2010 hadi 2015, kasi ya maambukizi mapya imepungua kwa asilimia 20.

0 Responses to “ IDADI YA WATANZANIA WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI”

Post a Comment

More to Read