Tuesday, March 18, 2014

ATC KUANZISHA SAFARI MBEYA- DAR.





Shirika la ndege Tanzania (ATC) linatarajia kuanza safari zake kati ya mbeya na dare s salaam kuanzia  leo likitumia ndege ya kisasa ya CRJ – 2200 yenye uwezo wa kubeba abiria 50.

Meneja wa ATC Mkoa wa mbeya shabani mtambalike amesema ATC itazindua huduma zake leo katika uwanja wa kimataifa wa songwe  na kwamba itafanya safari zake mara nne kwa wiki.

Amesema matarajio yake ya baadaye ni kuwa na safari kwa siku zote za wiki na hatimaye kuanza safari za nchi jirani za Malawi , Zambia  na jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa kongo(DRC).

Mtambalike amesema ATC kwa sasa inamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na kuwa ndege hiyo ya CRJ-2200 inatumia injini ya jeti hivyo inao uwezo mkubwa na itakuwa inatumia muda wa saa  moja kutoka dar  es salaam kufika mbeya

0 Responses to “ATC KUANZISHA SAFARI MBEYA- DAR.”

Post a Comment

More to Read