Thursday, March 20, 2014
MGOGORO ZIWA NYASA SASA KUAMULIWA LEO MAPUTO.
Do you like this story?
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe |
Maamuzi ya mwisho ya usuluhishi wa mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya
Tanzania na Malawi yanatarajiwa kutolewa kesho na kutwa.
Mchakato wa kesi yake hadi sasa
umedumu kwa takribani miaka miwili sasa.
Maamuzi ya mwisho ya usuluhishi
huo yanatarajiwa kufanywa na jopo linaloundwa na Marais wastaafu watatu kutoka
nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini na Mashariki mwa Afrika ambao ni
Mwenyekiti waka ni Joachim Chissano (Msumbiji), Thabo Mbeki (Afrika Kusini) na
Festus Mogae (Botswana), huku wakishirikiana na wanasheria na wataalam wa
masuala ya migogoro ndani ya jumuiya hiyo.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar
es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga, alisema jopo hilo la usuluhishi wa
mpaka kati ya Tanzania na Malawi, katika Ziwa Nyasa, linatarajia kutoa taarifa
rasmi ya usuluhishi kwa siku mbili mfululizo kuanzia kesho hadi kesho kutwa
katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.
Mbali na jopo hilo, pia mawaziri
wa Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kutoka nchi za Tanzania
na Malawi, wanatarajia kuhudhuria kikao hicho nyeti cha siku mbili kwa ajili ya
kupokea taarifa hiyo ya maamuzi ya mwisho ya usuluhishi.
Jopo la wataalam na wanasheria wa
masuala ya mipaka toka ndani ya jumuiya hiyo ambao watashirikiana na Marais hao
wastaafu katika kutoa hatima ya usuluhisho huo linaundwa na Jaji Raymond
Ranjeva, Jaji mstaafu wa ICJ; Profesa George Kanyeihamba, Jaji mstaafu wa
Mahakama Kuu ya Uganda na Jaji Baney Afako, Mshauri wa Masuala ya Sheria kwenye
Umoja wa Afrika kuhusu mgogoro wa mpaka wa Sudan.
Wengine ni Profesa Martin Pratt,
Mkurugenzi wa Utafiti wa Jiografia na Mipaka; Dk. Dire David Tladi, Mjumbe wa
Kamisheni ya Sheria ya Umoja wa Mataifa; Miguel Chissano, Kiongozi wa Chuo
kinachoshughulikia mipaka ya Baharini na Nchi Kavu pamoja na Dk. Gbanga
Oduntun, Profesa wa Sheria na Mjumbe wa Kamisheni ya mgogoro wa mpaka kati ya
Nigeria na Cameroon.
Kabla ya kufanyika kwa matukio
hayo mawili mjini humo mwezi uliopita, Tanzania na Malawi kwa nyakati tofauti,
ziliitwa na jopo hilo kuhojiwa juu ya taarifa zao za ushahidi wa umiliki halali
wa ziwa hilo zilizowasilisha kwao na mawaziri wa mambo ya nje na wa pande hizo
mbili Novemba, mwaka jana.
Julai, mwaa juzi, Rais wa Malawi,
Joyce Banda, mara baada ya kuapishwa kushika kiti hicho kufuatia kifo cha
mtangulizi wake, Bingu wa Mutharika, aliibua mgogoro huo kwa kutoa leseni kwa
kampuni mbili za kigeni, kutafuta mafuta katika eneo la Ziwa ambalo
linamilikiwa na Tanzania, kwa madai ya kwamba ziwa hilo lote lipo upande wake
.
Mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya
Tanzania na Malawi, unaotambuliwa na sheria za kimataifa ni ule unaopita kati
ya ziwa hilo, ambao ulianza kutumiwa na raia wa nchi hizo mbili miaka mingi
iliyopita kwa kila upande kumiliki asilimia 50 ya Ziwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MGOGORO ZIWA NYASA SASA KUAMULIWA LEO MAPUTO.”
Post a Comment