Thursday, March 20, 2014
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UKAGUZI WA LESENI ZA BIASHARA.
Do you like this story?
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo. |
Serikali ilirejesha utaratibu wa
kupata leseni ya biashara kwa kulipia kuanzia 1/7/2013. Wizara ilitoa kipindi
cha miezi 6 kwa wafanyabiashara waliokuwa na leseni zisizo na ukomo kuhuisha
leseni zao. Kipindi hicho cha miezi 6 kiliishia 31/12/2013.
Na kama tulivyowatangazia Umma,
wale waliochelewa kufanya hivyo walipata leseni zao kwa kulipa ada na adhabu
kwa mujibu wa Sheria ya Leseni Namba 25 ya 1972 kifungu cha 11(a) na (b).
Ukaguzi: (Kifungu na 17 cha Sheria Na 25 ya 1972) Ukaguzi unafanyika ili kuhakikisha
kuwa biashara zinafanyika kwa mujibu wa Sheria na taratibu za nchi.
Kama alivyoagiza KMWVB, kwamba
Mamlaka za Leseni zifanye ukaguzi wa kina katika maeneo yao, tunapenda
kusisitiza kuwa ukaguzi huu ufanyike kati ya mwezi wa Aprili na Mei. Wito kwa
wananchi Wananchi kufuata Sheria na taratibu za nchi, kwani kufanya hivyo ni
alama ya maendeleo. Kigezo kimoja cha kupima maendeleo ya watu, ni kwa jinsi
gani watu hao wanafuata taratibu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UKAGUZI WA LESENI ZA BIASHARA.”
Post a Comment