Tuesday, April 29, 2014
ASKARI SITA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOANI MBEYA WAFUKUZWA KAZI KWA RUSHWA.
Do you like this story?
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya
limewafukuza kazi Askari 6 wa kikosi cha Usalama barabarani Wilaya za
Rungwe na Mbeya kwa tuhuma za kuomba,kushawishi na kupokea rushwa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya
Ahmed Msangi amewatataja Askari hao kuwa ni pamoja na waliokuwa wakifanya
kazi wilaya ya Mbeya barabara ya Mbeya/Tunduma eneo la Songwe ni Copro
Jonson,PC Rymond na PC Simon.
Msangi amewataja wengine kuwa ni pamoja
Sajini Hezron,PC Shaban na PC Kajolo ambao walikuwa wanafanya kazi barabara ya
Mbeya/Rungwe wilaya ya Rungwe.
Askari hao walikuwa wanakabiliwa na
makosa hayo na walifikishwa katika Mahakama ya Kijeshi na Hukumu kutolewa
Aprili 24 mwaka huu na kupewa adhabu ya kufukuzwa kazi.
Aidha Kamanda Msangi amesema Jeshi lake
halitasita kuwafukuza kazi Askari watakaokwenda kinyume na maadili ya Jeshi la
Polisi na Askari yeyote atakayekwenda kinyume atakumbwa na adhabu kali ikiwa ni
pamoja na kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani.
Askari wengine waliofukuzwa kazi hivi
karibuni ni pamoja na PC James Kagomba ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 30
jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha,WP Prisca Kilwai
anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mtoto.
Wengine wliohukumiwa kifungo cha mwaka
mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia ni DC Marcelino Venance
mwenye namba 8084,PC Juma Idd mwenye namba 3117 na Askari wa Mgambo MG Jackson
Mwakalobo ambao walidaiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi Dentho Kajigili
aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Ivumwe ya Jijini Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ASKARI SITA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOANI MBEYA WAFUKUZWA KAZI KWA RUSHWA.”
Post a Comment