Tuesday, April 29, 2014
MKOA WA NJOMBE BADO UNAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI.
Do you like this story?
Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi [VVU] Nchini Tanzania bado ni tishio
na mkoa wa Njombe unaendelea kuongoza kwa kuwa na maambukizi ya asilimia
kubwa zaidi.
Njombe inaongoza kwa asilimia 14.8 kati ya mikoa kumi yenye maambukizi.
Njombe inaongoza kwa asilimia 14.8 kati ya mikoa kumi yenye maambukizi.
Mikoa mingine ni Iringa asilimia 9.1, Mbeya asilimia 9.o,
Shinyanga asilimia 7.4, Ruvuma asilimia 7.0, Dar es salaam asilimia 6.9,
Rukwa asilimia 6.2, Katavi asilimia 5.9, Pwani asilimia 5.9 na Tabora
asilimia 5.1.
Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti wa Tume Ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi [Tacaids] Dk Raphael Kalinga amesema utafiti wa maambukizi ya VVU Kwa wanaume na wanawake Tanzania bara wenye umri wa kati ya miaka 15 na 45 ni asilimia 5.3 .
Kundi linalo ambukizwa zaidi ni akina mama likifuatiwa na vijana na mikakati zaidi ya makundi hayo inaendelea kuboreshwa ili kupunguza maambukizi kwa makundi hayo.
Dk Raphael Kalinga Amesema asilimia 98 ya Watanzania wanafahamu ugonjwa wa Ukimwi lakini kati yao ni asilimia 60 tu ya wanaoelewa namna ya kujikinga na maambukizi hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKOA WA NJOMBE BADO UNAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI.”
Post a Comment