Tuesday, April 29, 2014
BREAKING NEWS: BASI LA SUMRY LAUA KWA KUGONGA WATU 13 AKIWEMO ASKARI WA USALAMA BARABARANI SINGIDA USIKU HUU.
Do you like this story?
WATU 13 akiwemo askari wa kikosi cha
usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya
Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani
Singida usiku huu.
Ajali hiyo imetokea baada ya ajali ya
kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha
papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku
trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na
kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza
maisha eneo hilo.
Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma
kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda
kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida.
Miili 14 ya waliopoteza maisha katika
ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na
majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI
PEMA PEPONI. AMEN!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BREAKING NEWS: BASI LA SUMRY LAUA KWA KUGONGA WATU 13 AKIWEMO ASKARI WA USALAMA BARABARANI SINGIDA USIKU HUU.”
Post a Comment