Friday, August 15, 2014
IKULU YATOA TAMKO KUHUSU UKAWA.
Do you like this story?
KURUGENZI
ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imesema Rais Jakaya Kikwete hana mamlaka ya
kusitisha Bunge Maalumu la Katiba kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba.Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu, Bw.Salva Rweyemamu,
aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Bw. Rweyemamu alikuwa akikanusha taarifa iliyoandikwa na gazeti
moja linalotoka mara moja kwa wiki ambalo liliandika habari iliyobeba kichwa
cha habari “Rais Baraka Obama amgeuka JK”.
Alisema
Rais Kikwete hana mamlaka ya kusitisha Bunge hilo kwani Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba haijampa mamlaka hayo hivyo ni vyema watu wakaisoma sheria hiyo na kuielewa.
Aliongeza
kuwa, sheria hiyo haitoi nafasi kwa mtu mwingine kulivunja Bunge hilo bali
tofauti zilizopo watazimaliza wenyewe akiwataka wajumbe wa Bunge hilo
waliosusia vikao kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), warejee
bungeni kuendelea na vikao ili wananchi wapate Katiba Mpya.
Akizungumzia
taarifa iliyoandikwa na gazeti hilo, alisema habari hiyo haina ukweli bali
imetungwa kwani katika mkutano uliofanyika Mjini Washington D.C, nchini
Marekani hivi karibuni, masuala hayo hayajazungumzwa kama inavyodaiwa.
Habari hii ilikuwa ikisema Rais Barack
Obama wa Marekani amemuuliza Rais Kikwete kuhusu fedha za Kampuni ya Kufua
Umeme ya IPTL zilizochukuliwa kutoka Benki Kuu nchini (BoT)
alisema.
Alisema
katika mkutano uliowakutanisha viongozi mbalimbali, hakuna jambo la IPTL ambalo
lilizungumzwa ambapo Rais Kikwete alikutana na Mtendaji Mkuu wa Shirika la
Misaada la Maendeleo nchini Marekani la Millennium Challenge Corporation (MCC)
na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Aliongeza
kuwa, Rais Kikwete pia alizungumza na Rais wa Malawi, Peter Mutharika ambaye
alimkaribisha nchini kwake ili wakale samaki wa ziwa Malawi linalojulikana kama
ziwa Nyasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “IKULU YATOA TAMKO KUHUSU UKAWA.”
Post a Comment