Friday, August 15, 2014
WATU NANE WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA MWL.NYERERE WAKIINGIA NCHINI KWA PASPOTI BANDIA ZA MATAIFA TOFAUTI YA ULAYA
Do you like this story?
Idara ya
Uhamiaji Nchini, imewakamata Raia wa nane (8) wa kigeni wakati wakiingia
nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere, wakiwa
na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya.
Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014 majira ya
saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la Ndege la
Uturuki yenye Namba TK 603, wakitokea Uturuki na kujitambulisha
kuwa Raia wa Sweden na Belgium.
Maofisa
Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia ukaguzi wa
kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu kuingia nchini
Tanzania na pasipoti za bandia.
kukamatwa kwa
wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji haramu nchini
ambapo suala la Udhibiti wa Mipaka linapewa kipaumbele.
akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji
Tatu Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji
wanaendelea kufanyakazi usiku na mchana kuhakikisha Sheria
na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa. "Idara ya Uhamiaji, iko
macho hatulali kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa nchi ikiwa ndio jukumu letu
namba moja unaimarika. kwahivyo, kila mtu awe Raia wa kigeni na
Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na Taratibu zilizopo za kuingia
na kutoka nchini" .
Hadi sasa,
Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea kushikiliwa na Maofisa wa
Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri kurudishwa
walikotoka. Hili ni wimbi lililoibuka hivi karibuni kwa baadhi
ya Raia wa nchi za Iraq, Iran, Syria kujaribu kuingia nchini isivyo halali
huku ikisemekana lengo lao kubwa ni kuingia Tanzania na baadae kutoka kuelekea
Mataifa ya Ulaya.
Majina ya
Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina halisi
na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye
mabano ni kama ifuatavyo;
1. ADEL SHAALAN
MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam.
G1489664)
2. SAMER
HELMI KAMIT - SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA
HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
3. MOHAMMED
JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
4. DAVID
GABRIEL POBLETE - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT
NO. A 4910203)
5. SADDAM
ALKHAMERI AREF - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN,
PPT. NO. G 1489664)
6. ALI
MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
7. OSAMAH
ZAID GHAEB AL-OBAIDI - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
8. ALI
HUSSEIN OLEIWI - IRAQ, PPT. NO. G 1111623
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATU NANE WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA MWL.NYERERE WAKIINGIA NCHINI KWA PASPOTI BANDIA ZA MATAIFA TOFAUTI YA ULAYA ”
Post a Comment