Friday, August 15, 2014

JAMAA ATEMBEZWA UCHI MTAANI BAADA YA KUMTAKA MWANAUME MWENZIE AMLAWITI




Na Saimeni Mgalula,Mbeya

Matukio ya kulawitiana yameendelea kuchukua sura mpya baada ya mkazi mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa wa mtaa wa Maporomoko uliopo katika mji mdogo wa Tunduma uliopo Wilaya ya Momba Mkoani hapa,ametembezwa uchi wa mnyama mjini baada ya yeye mwenyewe kutaka kulawitiwa na mwanamume mwenzake ambaye naye jina tunalihifadhi.

Tukio hilo lilitokea juzi huko mtaani na mbinu waliotumia ili kumkamata ni mmoja kati yao kukubali kitendo hicho cha ajabu cha ulawiti baada ya kushawishiwa sana bila kujua kuwa mwenzake ameshaandaa watu ili wamuumbue kwa hilo.


Aliendelea kwa kusema kuwa mmoja huyo alianza kwa kumuandikia sms ya kusema kuwa anataka amuingize kwenye ulimwengu wa mapenzi kitu kilicho mshtua mwanaume huyo ambaye alikuwa anatongozwa na mwanaume mwenziye ili akamlawiti.

Aidha alisema kuwa aliamua kukubali na kumchukua kwenda naye kwenye chumba chake alichopanga ili waanze kazi baadaya ya yule mwanaume kutoa nguo zote mwenzake akapiga simu kwa mwenzake ambaye alikuwa anakaa naye pale ambaye alitambulika kwa jina moja la Asifiwe ili wamuumbue.

Asifiwe aliwaita watu wengi waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya kumshikisha adabu njemba hiyo inayotaka kulawitiwa ndipo akafumaniwa na kula kichapo cha hali ya juu na wakaamua kumtembeza uchi mtaa mzima.
tulijaribu kumtafuta mtuhumiwa kwa bahati mbaya hatukuweza kumpata kutokana na kuzingirwa na umati wa watu ili aeleze sababu zilizo mfanya atake kufanya hivyo.

Na kwa upande wa mashuhuda walisema kuwa labda ni masharti ambayo atakuwa amepewa na mganga wa kienyeji kutokana na mali alizokuwanazo ili zizidi kuongezeka basi afanye mchezo huo mchafu.

0 Responses to “JAMAA ATEMBEZWA UCHI MTAANI BAADA YA KUMTAKA MWANAUME MWENZIE AMLAWITI ”

Post a Comment

More to Read