Friday, August 15, 2014

PATRICK PHIRI ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA, ASEMA AMEKUJA KUREJESHA MATAJI……




Kuwasili nchini kwa kocha raia wa Zambia klabuni, Simba SC siku ya jana ni kama kume ‘ wachengua’ mashabiki wengi wa timu hiyo. Kocha huyo hataki kuonekana kama ‘ kiraka wa muda’ na anataka kuwa katika mipango ya muda mrefu ambayo itakuwa na mafanikio. ” Nimerudi tena Simba kurejesha heshima na mafanikio yaliyopotea” alisema, Phiri kocha ambaye aliipatia timu hiyo ubingwa bila kupoteza mchezo wowote msimu wa 2009/10.
Phiri anakuwa mwalimu wa tano sita kufanya kazi klabuni hapo tangu, Mei, 2011, Milovan Curkovic pekee alifanikiwa kushinda ubingwa wa Bara msimu wa 2011/12 msimu ambao Simba ilifundishwa na makocha wawili baada ya kufutwa kazi kwa Mganda, Moses Basena baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza. Akiwa na matarajio makubwa ya kupata ushirikiano kutoka kwa wachezaji, viongozi na mashabiki, Phiri ametoa ahadi ya kuurejesha ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.


Patrick Phiri akisaini mkataba wa mwaka mmoja leo hii mbele ya rais wa klabu ya Simba Evans Aveva pamoja na mjumbe wa kamati ya utendaji Colin Fritch,anayeshuhudia ni meneja wa Phiri ambaye pia ni mtoto wake, Melesiana Phiri.

” Nitaipa Simba ubingwa wa ligi kuu msimu ujao” alisema maneno hayo kwa kujiamini licha ya kutambua kuwa timu nyingine zimejiandaa vya kutosha huku makocha kama, Patrick Omog wa Azam FC na Marcio Maximo wa Yanga SC wakinoa na kuwekeza mbinu na ufundi katika vikosi vyao kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa. Mashabiki wa Simba wamefurahi kuona mwalimu huyo aliyewapa ubingwa mwaka 2004 akirejea na hivyo pia kwa Phiri ambaye ameushukuru uongozi wa klabu hiyo kumuamini na kumrejesha Tanzania sehemu anayosema ni ‘ nyumbani kwake kwa pili baada ya nchi yake ya Zambia’
. ” Tanzania ni nyumbani kwangu, nafurahi kurudi kufanya kazi katika nchi hii ambayo naichukulia kama nchi yangu ya pili “.
Phiri alizungumza maneno hayo mara tu baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha timu hiyo yenye maskani kwenye mitaa ya msimbazi jijini Dar Es Salaam.

0 Responses to “PATRICK PHIRI ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA, ASEMA AMEKUJA KUREJESHA MATAJI……”

Post a Comment

More to Read