Friday, August 1, 2014

KOVA AWATAKA MADEREVA KUKATAA KUTOA RUSHWA.




KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna (CP), Suleiman Kova, amewataka madereva wanaoendesha vyombo vya moto, kutoa taarifa za askari wanaodai rushwa pindi wanapobainika na makosa ya uvunjifu wa sheria za barabarani.

Kauli hiyo ya Kova, imekuja baada ya baadhi ya madereva kutoa malalamiko yao katika  vyombo vya habari, kwamba baadhi ya askari polisi wamekuwa wakiacha idara zao za kazi na kukimbilia barabarani kutafuta rushwa.

Kamanda Kova alisema endapo kutakuwa na askari anadai rushwa, dereva huyo asitoe, bali achukue jina na namba za askari huyo ambazo zipo kifuani na kuripoti polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa askari huyo.

“Endapo askari polisi watadai rushwa, kataeni msitoe na chukueni namba zao na majina yao mnirushie, mimi nitawashughulikia kisheria, sheria hairuhusu kutoa wala kupokea rushwa,” alisisitiza Kova.

Akizungumzia askari wanaoacha idara zao na kukimbilia barabarani kukamata magari, alisema hali hiyo inasababishwa na uhaba wa askari wa usalama barabarani, hususan kukiwa na foleni, hivyo wakati mwingine wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza ajali zisizotarajiwa barabarani.

0 Responses to “KOVA AWATAKA MADEREVA KUKATAA KUTOA RUSHWA.”

Post a Comment

More to Read