Thursday, October 30, 2014
29 WAITWA KIKOSI CHA MABORESHO TAIFA STARS
Do you like this story?
Na
Boniface Wambura, Dar es salaam
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia kuendelea na awamu ya pili ya
maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars) inayojumuisha vijana wenye umri chini
ya miaka miaka 23.
Katika awamu
hii, Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ameteua majina ya wachezaji 29 ambao
watakuwa wakiingia kambini mara moja kwa mwezi siku ya Jumapili baada ya
kuwakilisha timu zao kwenye mechi za ligi.
Kikosi
hicho cha maboresho kitakuwa kikifanya programu maalumu za mazoezi mpaka siku
ya Jumatano na kucheza mechi za kirafiki na timu za ndani au nje ya nchi.
Lengo
hasa la programu hiyo ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji ambao
walipatikana katika awamu ya kwanza ya mpango wa maboresho mwanzoni mwa mwaka huu
Tukuyu mkoani Mbeya, lakini wamekuwa hawatumiki. Pia kuwandaa vijana ili
kujenga timu ya ushindani na imara ya Taifa ya muda mrefu.
TFF ina
imani kubwa kuwa programu hii itakuwa na manufaa kwa soka ya Tanzania. Timu
hiyo itaingia kambini kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka huu katika hoteli
itakayotangazwa baadaye.
Wachezaji
walioteuliwa ni Aishi manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Aboubakar
Ally (Coastal Union), Miraji Adam (Simba), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Gadiel
Mbaga (Azam), Emmanuel Semwanda (African Lyon) na Joram Mgeveke (Simba).
Edward
Charles (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kassim Simbaulanga (African
Lyon), Pato Ngonyani (Yanga), Adam Salamba (Kahama), Hassan Banda (Simba),
Mohamed Hussein (Simba), Hashim Magoma (Stand United), Makarani Ally (Mtibwa
Sugar), Said Juma (Yanga) na Said Hamis (Simba).
Aboubakary
Ally Mohamed (Zanzibar), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Malombe (Geita Gold),
Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda
SC), Kelvin Friday (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Alfred Masumbakenda
(Kahama) na Simon Msuva (Yanga).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “29 WAITWA KIKOSI CHA MABORESHO TAIFA STARS”
Post a Comment