Wednesday, October 29, 2014

UMEIPATA HII YA KILA MTANZANIA KUPATA SMARTPHONE YA BURE?








Headline yake tu hii stori kwenye gazeti la Uhuru kwamba ‘Kila Mtanzania kupata simu ya kisasa bure‘ ndio imenifanya nihamasike kusoma kilichoandikwa ndani ambapo kwenye sentensi ya kwanza inasema >> kila
Mtanzania atakua na uwezo wa kupata simu ya kisasa ‘smart phone’ kwa
bei ya chini kabisa katika miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2020.


Hii ni moja ya mipango ya kampuni mpya ya simu iitwayo Viettel
inayomilikiwa na jeshi la Vietnam inayojiandaa kuingia kwenye soko la
simu Tanzania ambapo imemwambia Rais Kikwete juzi kwamba itateremsha kwa
kiasi kikubwa bei ya simu za kawaida na smart phone ili kila Mtanzania
awe na simu




Imesema pia itasambaza mawasiliano ya Internet kwa kila kijiji
Tanzania na taasisi za umma kama shule, hospitali na vituo vya Polisi,
zitapatiwa huduma hii bila malipo yoyote.


Kingine
walichokisema ni kwamba wanataka kupunguza bei ya simu za kawaida
kufikia elfu 25 za Kitanzania na bei ya smart phone kufikia elfu 65 za
Kitanzania ambapo pia wamekaririwa wakisema >>> ‘tunataka
kuifanya bei ya kununua smart phone kuwa mara 10 chini ya bei ya
kununulia computer, tunakusudia pia kupunguza bei ya matumizi ya simu
kwa dola moja sawa na shilingi 1600 kwa watu wa kawaida kwa mwezi, kwa
wale wanaotumia huduma nyingi zaidi watalipa shilingi elfu 78 kwa mwezi‘

Kwa kumalizia, unaambiwa ndani ya miaka mitatu ya kampuni hiyo kuanza
kufanya kazi Tanzania, vijiji 4000 ambavyo sasa hivi havina mawasiliano
vitapatiwa hiyo huduma kwa awamu ya kwanza.

 


0 Responses to “UMEIPATA HII YA KILA MTANZANIA KUPATA SMARTPHONE YA BURE?”

Post a Comment

More to Read