Tuesday, October 21, 2014
KITUO KIPYA CHA DALADALA UBUNGO KUZINDULIWA KESHO ALHAMISI
Do you like this story?
Kituo kipya cha daladala cha Ubungo kilichohamishiwa Kituo cha Simu, kati
ya barabara ya Sam Nujoma na Sinza jijini Dar es Salaam, kinatarajiwa
kuzinduliwa rasmi kesho kutwa (Alhamisi).
Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Daladala zinazotoka Masaki zikifika barabara ya Shekilango zitaingia kulia kwa kutumia barabara ya Tanesco inayokwenda moja kwa moja kituoni Simu 2000 na zitarudi barabara ya Shekilango kwa kutumia njia hiyo hiyo ya Tanesco.
Zinazotoka Kariakoo, Posta na Kariakoo zikifika mataa ya Ubungo zitaingia kulia (barabara ya Sam Nujoma) kwenda kituoni Simu 2000, zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo hiyo.
Aidha, kwa daladala zinazotokea barabara ya Mandela, madereva wake wameelekezwa; Kuvuka mataa ya Ubungo (kwa kutumia barabara ya Sam Nujuma) na kwenda kituoni Simu 2000, zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo hiyo.
Zinazotoka Mwenge zikikaribia Jengo la Mawasiliano Towers zitachepukia kushoto kwa kutumia barabara ya akiba inayopita mbele ya Mawasiliano Towers hadi kituoni Simu 2000, zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara ya Sam Nujoma.
Na zile zinazotoka Kimara na Mbezi, zikifika mataa ya Ubungo zitaingia kulia kwenda kituoni Simu 2000. zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo hiyo.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ KITUO KIPYA CHA DALADALA UBUNGO KUZINDULIWA KESHO ALHAMISI ”
Post a Comment