Thursday, October 2, 2014
MICHUANO YA WAZI GOFU KUTIMUA VUMBI OKTOBA 4
Do you like this story?
Meneja Biashara wa kampuni ya UAP Insurance Tanzania inayoratibu michuano hiyo Raymond Komanga akizungumza na waandishi wa Habari. |
Mashindano ya wazi ya gofu ya Arusha gofu
championships yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 4 mwaka huu katika
uwanja wa gymkhana jijini Arusha,
UAP ambao
ni kampuni la huduma ya utoaji Bima, uwekezaji na utawala, uwekezaji wa vitega
uchumi na maendeleo, pamoja na kuwa washauri katika mambo ya fedha na ulinzi wa
mali, ndio waandaaji wa mchuano huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam
meneja biashara wa kampuni ya UAP Insurance Tanzania inayoratibu michuano hiyo
Raymond Komanga alisema wanatarajia kushirikisha wachezaji wa gofu wa rika zote
kutoka jijini humo na hata maeneo mengine ya jirani
Komanga alisema lengo la michuano hiyo ni pamoja
na kuwashukuru wakazi wa jiji la Arusha kutokana na ushirkiano wao na kampuni
hiyo.
Wachezaji watakaojitokeza kushiriki katika mashindano
haya watanufaika kutokana na kwamba watakuza vipaji vyao,
kujenga afya pamoja na kukuza wigo wao wa washiriki wa kibiashara kupitia
mchezo wa gofu, hivyo tunaomba wachezaji gofu wajitokeze siku hiyo.
Kwa sasa UAP inafanya kazi katika
nchi 6 Afrikazikiwemo Kenya, Uganda, South Sudan, Rwanda, DRC na Tanzania. Baadhi ya
bidhaa na huduma za UAP ni pamoja na Bima ya mazao , Bima Mifugo , Bima ya
magari, Bima ya mabasi na lori , Bima ya Ndani, bima ya matibabu, bima shule ,
dhima ya umma , bima ya ajali ya makundi au binafsi , bima yamoto na hatarizingine
na mengine zaidi.
Komanga alisema lengo lingine ni kutaka kuona
michuano hiyo inapata washiriki wengi ili kutoa ushindani na kwamba huo ni
mwanzo kwani bado watandaa michuano mingine.
Tutahakikisha
tunaandaa michezo mbalimbali ikiwemo huu wa gofu na ipo lingine la kuandaa jijini Arusha ni kuhakikisha
inakuwa na wachezji wengi wazuri mchezo
huo ambao baadaye wataweza kuichezea timu ya taifa na klabu mbalimbali8
alisema.
Alisema mshindi wa kwanza katika michuano hiyo
atapata zawadi ya kulipiwa bima ya nyumba anayoishi pamoja na watu wawili
anaoishi nao pili atalipiwa bima ya gofu kwa mwaka mmoja wakati mshindi wa tatu
atalipiwa bima ya ajali ya aina yoyote ndani ya mwaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MICHUANO YA WAZI GOFU KUTIMUA VUMBI OKTOBA 4”
Post a Comment