Tuesday, October 21, 2014
OSCAR PISTORIUS AFUNGWA JELA MIAKA MITANO
Do you like this story?
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5
baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji
bila ya kukusudia.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo, Thokozile Masipa, alianza kutoa kauli yake ya
mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto
kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.
Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10
gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi
alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka ulisisitiza Pistorius afungwe jela wakati wakili wa
Pistorius wakimtaka jaji ampe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia
apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.
Jaji alisema kuwa Pistorius asingepewa adhabu ya kifungo cha nyumbani
kwani hukumu kama hiyo ingekuwa hatua mbaya na mfano mbaya kwa wahalifu.
CHANZO:BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ OSCAR PISTORIUS AFUNGWA JELA MIAKA MITANO ”
Post a Comment