Wednesday, April 15, 2015
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA.
Do you like this story?
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi |
WAFANYABIASHARA Mkoani Mbeya, wameshauriwa kufunga kamera
za CCTV katika maeneo yao ya biashara.
Ushauri huo umetolewa leo na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Mbeya, Ahmed Msangi, kutokana na kushamiri kwa vitendo vya uhalifu,
vinavyoambatana na wizi wa kutumia silaha
Msangi, amelazimika
kulizungumzia hilo, baada ya kutokea kwa tukio la wizi wa silaha, bidhaa na
fedha za mauzo lililotokea mwishoni mwa mwezi huu katika moja ya duka lililopo
ndani ya Jiji la Mbeya na kwamba uhalifu huo ulifanywa na wanawake.
Amesema kuwa, wanawake hao ambao ni mama lishe waliingia
ndani ya duka moja lililopo Jijini hapa na kufanikiwa kuiba bastola moja na
mali kisha kukimbia, lakini kamera za CCTV zilizofungwa ndani ya duka hilo
ziliweza kuwanasa.
Hata hivyo,Msangi amesema kuwa polisi inawatafuta watuhumiwa
hao kwani baada ya kubaini kuwa wanatafutwa walitelekeza bastora hiyo kutoroka,
mbali na kufanya uhalifu kwenye duka hilo pia wamewaliza watu wengi.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA.”
Post a Comment